Header Ads Widget

IDADI YA VIFO VYA AJALI TANGA YAONGEZEKA YAFIKIA 20

 


NA AMINA SAID,MATUKIO DAIMA TANGA.

Ajali ya magari kugongana uso kwa uso n kusababisha Vifo vya watu 20   huko Jijini Tanga imeleta simanzi na majonzi kwa Wananchi huku Serikali ikiwa mstari wa mbele katika kuwafariji.


Katika ajali hiyo iliyotokea kijiji cha Gereza iliyohusisha gari aina ya Coaster iliyokuwa ikisafirisha maiti na Fusso kuelekea mkoani Kilimanjaro tayari Viongozi mbalimbali wa Serikali wamefika eneo la tukio.


Rais Samia Suluhu Hassan akitoa salaam za pole na maagizo kadhaa kufuatia tukio hilo la ajali ambayo imejeruhi watu wapatao 12 wakiwemo 14 wa familia moja.


Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya mapinduzi Zanzibar,Hemed Suleiman Abdulla aliyepo mkoani Tanga, asubuhi saa 3.00 asubuhi alilazimika kukatiza ziara yake na kwenda kuwaona na kuwafariji majeruhi waliolazwa hospitali ya Bombo.


Mganga mfawidhi wa hospitalini ya rufaa ya Bombo, Dk. Naima Yusuph amethibitisha kuwapokea majeruhi 12 na wawili waliotegemewa kupelekwa muhimbili kati yao wawili wamefariki dunia ambao wamefikisha idadi ya watu 19 waliofariki kwenye ajali hiyo.


Aidha,alieleza kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika hospital ya Magunga iliyopo wilayani Korogwe mkoani Tanga.


Akiwa katika mwendelezo wilayani Pangani Makamu wa pili wa Rais wa Serikali ya Zanzibar aliendelea kuwapa pole wale wote waliofikwa na msiba huo.


Kamishna wa operesheni na mafunzo wa jeshi la polisi akithibitisha,CP Awadh Haji amefika akizungumza na waandishi hospital ya Magunga wilayani Korogwe mkoani Tanga akimwakilisha mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP.


CP Awadhi aliamctana na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani kamishna msaidizi...ambapo walipokelewa na kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Tanga.


Viongozi hao wamefanikiwa kufika eneo la tukio  huku kamisha Awadhi akiwaasa madereva kufuata sheria za usalama barabarani na kwamba jeshi halitasita kuchukua hatua stahiki kwa watakaokiuka.


CP Awadh akimwakilisha IGP Camilius Wambura ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa waliokumbwa na kadhia hiyo akiwataka kuwa na subira.


Mkuu wa mkoa wa Tanga,Omari Mgumba ambaye ni mwenyekiti ya ulinzi na usalama ameonekana kuwa mstari wa mbele muda wote kushughulikia changamoto hiyo iliyojitokeza.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS