Header Ads Widget

CITY COLLEGE MWANZA WATOA MSAADA KITUO CHA WATU WENYE MAHITAJI MAALUMU NA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU









NA CHAUSIKU SAID 

,MATUKIO DAIMAAPP MWANZA.


Chuo Cha Afya City College kimetoa msaada katika kituo Cha watu wenye magonjwa ya akili Bukumbi pamoja na shule ya Idetemya Kwa watoto waishio katika mazingira magumu Wilayani Misungwi Mkoani Mwanza.


Zabibu Urassa Mkurugenzi mtendaji wa city college ameeleza kuwa wameamua kurudisha shukrani Kwa jamii Kwa kutoa misaada Kwa watu wenye mahitaji maalumu na kufanya uzinduzi wa jogging club ambayo itawasaidia kutoa elimu juu ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili mashuleni.


"Tumeamua kuungana na kikindi chetu Cha jogging club Kwa ajili ya kuhamasisha jamii kuweza kushirikiana na serikali kusaidia watu wenye mahitaji maalumu na ukatili wa kijinsia" Alisema Zabibu.


Afisa Muuguzi kituo Cha watu mwenyewe magonjwa ya akili Kaliba Ngereja amekishukru chuo hicho na kuwataka watu kuendelea kunitoa na kuona watu wenye mahitaji maalumu wanahitaji misaada ili waweze kujiona wako sawa na watu wengine.


" Huu msaada tulioupata Leo ni mkubwa sana utatusaidia Kwa kiasi kikubwa katika kuendesha dhughuli za hapa kituoni kwetu"Alisema Ngereja.


Ngereja ameeleza kuwa changamoto kubwa katika kituo hicho ni ukosefu wa sabauni kutokana na uhitaji wa watu hao ni sabubi ili waweze kuwa safi na nadhifu.


"Kila siku lazima tutumie sabuni ya unga kuanzia kilo mbili Hadi tatu kutokana na watu Hawa kujisaidia kitandani na kujikojolea Kwa hiyo msaada huu utatusaidia sana" Alisema Ngereja.


Aidha amewataka watu binafsi na mashirika pamoja na taasisi mbalimbali kuendelea kujitolea Kwa watu wenye mahitaji maalumu.


Filimon John ni Afisa usitawi Jamii Wilaya ya Misungwi ameeleza kuwa jamii inapaswa kutambua bado Kuna makundi mengi yanahitaji misaada na serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha huduma zinawafikia watu wenye mahitaji maalumu.


"Tunaamini kabsa hata sisi ambao tunajiona tuko imara ni wazi kwamba Kuna kitu hatuwezi kukikamilisha bila msaada watu wengine" Alisema John.


John ameeleza kuwa makundi ya watu wenye mahitaji maalumu serikali peke yake hauwezi kuwa na uwezo wa kuweza kuwa hudumia peke yao hivyo taasisi, watu binafsi wanajukumu la kuwasaidia.


"Haya makundi ni mengi sana Wala sio kundi moja linahitaji msaada, Mimi ninaamini kabsa ni mengi" Alisema John.


Francis Mtembei Mratibu wa dawatinla jinsia City College ameeleza kuwa wanajukumu kubwa la kuhakikisha wanaungana na serikali ambayo inahimiza kushirikiana na watu wenye changamoto mbalimbali.


Mtembei Amesema kuwa kwenye jamii changamoto kubwa ambazo zinaikumba watu wengi ni swala la unyanyapaaji.


"Nakumbuka Rais wa jamhuri wa muungano wa Tanzania mwaka jana akiwa Dodoma bungeni  kitu kimona wapi alichokisema ni kwamba wizara inayohusika na maswala ya kijinsia ihakikishe inafika kwenye jamii kuhakikisha watu wanasaidiana nao" Alisema Mtembei.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS