Header Ads Widget

CHONGOLO AWANYOOSHEA KIDOLE WATENDAJI WA SERIKALI

 


Na Mwandishi wetu Morogoro


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Daniel Chongolo amewanyooshea kidole watendaji wa serikali kwa kuwa na tamaa za kutaka mafanikio ya haraka badala ya kkujiusisha na shughuri za utafutaji maendeleo katika maeneo ya kazi waliyopangiwa 


Akiongea na wakazi wa kata ya Dakawa Wilaya ya Morogoro  katika ziara yake ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama hicho Cha CCM Chongolo amesema wilaya hiyo imekuwa ikipitia migogoro ya Ardhi kutokana na baadhi ya watendaji kuwa wafugaji 


"Unakuta leo mtu anapewa kazi ya kuwa mtendaji wa Kata kesho unamkuta anamiliki ng'ombe ishirini, mshahara wake hata kwa mwaka hauwezi kumfanya  kuwa na Ng'ombe wawili,"amesema 


Na kuongeza Kusema  "Sasa niwatakeme  watendaji wote wa serikali kufanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya kazi yao ," amesema Chongolo



Hata hivyo pamoja na kuwataka watendaji kuzingatia maadilina Miikao ya kazi zao, amewataka wafugaji kuacha kupeana mialiko katika maeneo wanayopangiwa na serikali kwa ajili malisho.


"Ukiona kuna mgogoro wa Mkulima na Mfugaji maana yake kuna mtu hapo katikati anategeneza tatizo hivyo basi Serikali imekuwa ikiweka utaratibu wa mpango bora wa matumizi ya ardhi kwa kutenga maeneo kwa ajili ya  kilimo ,wafugaji,"


Nakuogeza Kusema"  Lakini kumekuwa changamoto kwa wafugaji wanaalikana wengi baadae eneo linakuwa dogo wanaingia kwa mkulima migogoro inaanza huku mkulima ukimpa eneo lake atalima kama alivyohitaji," amesema Chongolo.



Kutokana na hali hiyo Chongolo amemtaja Mkuu Wilaya ya  Mvomelo Dkt, Judith Lundi kuhakikisha  anapunguza migogoro ya wakulima na wafugaji katika Wilaya yake.


Awali Mbunge wa Jimbo hilo Jonas Vanzela ametoa malalamiko kuwa Wilaya hiyo imekuaa na migogoro ya wakulima na wafugaji pamoja na migogoro ya mipaka.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI