Header Ads Widget

UWANJA WA NDEGE WA BUKOBA WAFUNGULIWA RASMI

 .


NA TITUS MWOMBEKI, Matukio Daima App Kagera.

UWANJA wa ndege wa Bukoba umefunguliwa rasmi baada ya kufungwa kwa muda kutokana na ajali ya ndege iliyotokea Novemba 6 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 19.


Taarifa hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Chalamila wakati akiongea na waandishi wa habari baada ya kufika katika uwanja huo akiambatana na viongozi mbalimbali wa serikali.


“Nitumie nafasi hii pia kwa furaha kubwa kuwatangazia kuwa uwanja wa ndege wa Bukoba umekwisha funguliwa rasmi na tayari kutoka saa kumi na mbili leo asubuhi ya Novemba 9, 2022 safari za ndege zimeruhusiwa kuanza”


Aidha amewasihi wananchi naotamani kufanya safari zao  za ndege kuendelea kufanya hivyo na wasiogope kwa kilichotokea kwani ajali za ndege hazitokei mara kwa mara.



“Ajali za ndege hazitokei mara kwa mara kama ilivyo kwa gari au kifaa chochote, linapotokea jambo kama hili basi huwa ni mara chache sana tena ikiwezekana kwa miaka mingi mno kwahiyo niwatoe wasiwasi wananchi wote, hata mimi mwenyewe leo baada ya safari za ndege kuanza rasmi katika uwanja huu nitapanda kuelekea mahali ambapo sitaki kuwaambia naenda wapi”


Sambamba na hili amewaomba  waandishi wa habari kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi na kuwaeleza wananchi kuwa safari za ndege sasa zimeanza hivyo waendelee kupanda huku akisema kuwa kamwe ajali kama hii haitatokea kwani wamejipanga kutokana na kilichotokea.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI