Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango
akisalimiana na Mwenyekiti
wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Sheikh Alhad Mussa Salum wakati akiwasili katika Ukumbi
wa Mikutano
wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam
kufungua Kongamano
la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya
Maridhiano Tanzania
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango
akiwaongoza kuimba wimbo wa Taifa viongozi na washiriki wa Kongamano la Kitaifa
la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano
Tanzania wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika
katika Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es
salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango
akihutubia viongozi na washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa
Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania wakati wa Ufunguzi wa Kongamano hilo linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa
wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akikabidhi tuzo Mwenyekiti wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Sheikh Alhad Mussa Salum mara baada ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania linalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa
katika Picha ya pamoja na viongozi na wajumbe wa Kamati za Amani na Jumuiya ya
Maridhiano Tanzania mara baada ya kufungua Kongamano la Kitaifa
la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano
Tanzania linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano
wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango ametoa
wito kwa Viongozi wa dini zote, Viongozi wa Kimila na Wazee hapa nchini
kusaidia kulea watoto na vijana kimaadili ili kuweka mustakabali wa taifa na
watu wake kwenye mikono salama.
Makamu
wa Rais amesema hayo wakati alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa
la Maadili la Viongozi wa Dini wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano
Tanzania linalofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar
es salaam. Ameongeza kwamba vijana wakifundishwa mila na desturi sahihi na
kushika mafundisho ya dini, na wakawa na hofu ya Mwenyezi Mungu, maovu mengi
yatapungua hapa nchini.
Makamu
wa Rais amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Dini zote katika
kujenga maadili mema ndani ya jamii ya watanzania. Amewasihi viongozi wa dini kuendelea
kuliombea Taifa, viongozi na watumishi wa Serikali bila kuchoka ili kutekeleza vema
mipango ya maendeleo ya nchi na watu wake.
Aidha
Makamu wa Rais amekemea vikali ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto wa kike
na kiume hapa nchini na kuviagiza vyombo vya dola kuongeza nguvu katika
kupambana na ukatili huo. Aidha amewaasa walezi na wazazi kuweka mifumo imara
ya ulinzi kwa watoto katika ngazi ya familia, mtaa, mashuleni, madrasa, vyuoni na
sehemu nyingine ili kulinda haki na ustawi wa watoto na kuwaepusha na vitendo
vya ukatili vinavyofanyika dhidi yao.
Pia
amewakumbusha viongozi wa dini hapa nchini kukemea vitendo vya Rushwa na
Ufisadi kupitia nyumba za ibada pamoja na kuwaelimisha wananchi madhara ya
kutoa na kupokea rushwa na kushiriki kuhujumu mali za umma. Amesema Serikali itaendelea
kuimarisha mifumo ya utoaji huduma ili kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi
pamoja na kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayejihusisha
na vitendo hivi bila kujali cheo au nafasi yake katika jamii.
Halikadhalika
Makamu wa Rais amewasihi wazazi
na walezi kwa pamoja kushiriki katika mapambano ya kudhibiti matumizi ya dawa
za kulevya kwa kutoa elimu kwa jamii pamoja na kutoa
taarifa na kuwafichua wote wanajishughulisha na biashara hiyo haramu
inayoathiri afya za vijana hapa nchini.
Katika
hatua nyingine Makamu wa Rais amewaasa Viongozi
wa dini kujiepusha na migogoro ndani ya
Taasisi zao ambayo imekuwa ikisababishwa na uchu wa madaraka, ubinafsi, uchu wa fedha,
matumizi mabaya ya mali za taasisi za dini na ukiukwaji wa katiba za taasisi za
dini. Ametoa wito kwa viongozi hao wa dini kusuluhisha mapema migogoro ndani ya
taasisi zao inapojitokeza kwa kuzingatia
sheria, miongozo na taratibu zinazokubalika ili wawe mfano mzuri wa maadili kwa
jamii ya watanzania.
Kwa
Upande Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhandisi Hamad Masauni amesema Wizara hiyo
imeanzisha mfumo wa usajili na usimamizi wa jumuiya hpa nchini unaolenga
kusaidia changamoto mbalimbali ambazo zilikua zikilalamikiwa ikiwemo
ucheleweshaji wa usajili Jumuiya pamoja na kutopata taarifa mbalimbali. Amesema
mfumo huo utaimarisha usalama nchini kwa kukabiliana na Jumuiya zinazotumia mgongo wa dini katika kufanya
mambo ambayo ni kinyume na sheria za nchi.
Mwenyekiti
wa Kamati za Amani na Jumuiya ya Maridhiano Tanzania Sheikh Alhad Mussa Salum
amesema wataendelea kushirikiana na serikali katika kukabiliana na mmomonyoko
wa maadili uliopo hapa nchini. Amesema Taifa lolote hubebwa na maadili kama
heshima na utu wake katika uso wa dunia hivyo ni lazima viongozi wa dini
kusimamia jambo hilo kadri serikali itakavyokuwa ikielekeza.
Awali
akisoma Risala Katibu Mkuu, Jumuiya ya
Maridhiano Tanzania Mchungaji Dkt. Israel Maasa amesema Jumuiya hiyo imeweza
kufanya mambo mbalimbali ikiwemo kumaliza migogoro mbalimbali kati ya wakulima
na wafugaji, kupambana na mila potofu pamoja na kupambana na ukatili wa
kijinsia dhidi ya wanawake na Watoto.
0 Comments