NA HAMIDA RAMADHAN MATUKIO DAIMA App, DODOMA.
BODI ya usajili wa Wahandisi Nchini (ERB) imesema kuwa Katika Mwaka wa Fedha 2022/2023 inatarajia kujenga kituo kikubwa cha umahiri Jijini Dodoma ambapo ni moja ya vipaumbele vyake ili vijana waweze kufanya shughuli zao kwa kuonyesha ubunifu wao.
Msajili wa Bodi hiyo,Mhandisi Benard Kavishe ametoa taarifa hiyo jana Jijini hapa kwa Waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya ERB na Vipaumbele vyake kwa Mwaka wa fedha 2022/2023.
Sanjari na hilo,Mhandisi Kavishe alibainisha kuwa Bodi hiyo ina mpango wa miaka mitano kuanzia 2021 hadi 2025 ikiwa ni pamoja na kudhibiti Ukimwi pamoja na magonjwa ya kuambukiza na kupambana na rushwa.
Katika kuyaishi hayo,Alisema bodi hiyo imeweka kipaumbele kuwajengea uwezo wataalam wa ndani wa kada ya Uhandisi kwa kuratibu na kuendesha mafunzo endelevu ya ujuzi mbalimbali katika kutekeleza shughuli za kihandisi nchini.
Naye Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alieleza dhamira ya Serikali kupitia Bodi hiyo kuwa imewekeza fedha nyingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo na kwamba nchi imezalisha jumla ya wahandisi 33, 000 na baadhi yao 26 wameajiriwa huku wengine wakiendelea na masomo vyuoni ili kupata ujuzi zaidi.
Bodi ya Usajili wa Wahandisi ERB ilianzishwa Mwaka 1968 kwa mujibu wa Sheria namba15 kazi kubwa ni usajili Wahandisi na Kampuni na kudhibiti shughuli za kihandisi na lengo kubwa la Serikali ni kuangalia maslahi ya Umma hasa usalama kutokana na suala zima la udhibiti wa Bodi hiyo ambapo hadi Sasa ina jumla ya wahandisi zaidi ya elfu 30.
0 Comments