Watoto
wawili wa familia moja wamepoteza maisha papo hapo kwenye ajali iliyohusisha
magari matatu iliyotokea leo Jumatano Novemba 9, 2022 katika mteremko wa Iwambi
mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amethibitisha kutokea ajali hiyo.
Kuzaga amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:45 basi
aina ya Fuso namba T 601 DHC liligonga gari namba T 452 DHD Toyota Raum na kugonga
magari mengine huku chanzo cha ajali hiyo kikitajwa kuwa ni mwendokasi wa gari
hilo.
"Katika
ajali hiyo ni watoto wawili wa familia moja (waliokuwa katika gari dogo)
wamepoteza maisha, niendelee kuwaomba madereva kuwa waangalifu wanapokuwa
wanaendesha vyombo vya moto ili kuondokana na ajali hizi," amesema Kuzaga.
Baadhi ya
mashuhuda wa ajali hiyo wamesema tukio hilo lilitokea saa 12 asubuhi ambapo
dereva wa gari aina Fuso alijitahidi kumudu gari lake lakini alishindwa baada
ya kugongana ubavu na gari dogo.
Taarifa Zaidi
juu Habari hii utaipata kupitia Hotnews ya Matukio Daima Tv ifikapo saa 12:00
Jioni.
0 Comments