Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amezungumzia suala la mikutano ya vyama siasa, akisema inaleta ushindani, afya na demokrasia kwa Taifa.Mwaka 2016 Serikali ilipiga marufuku mikutano ya hadhara, baada ya kumalizika kwa uchaguzi ukuu wa mwaka 2015 ikieleza kuwa siasa hufanywa wakati wa uchaguzi.
Nape ambaye pia ni mbunge wa Mtamba mkoani Lindi ameyasema hayo leo Jumatatu, Oktoba 17, 2022 katika mahojiano maalumu katika kipindi cha ‘Joto Kali la Asubuhi’ kinachorushwa na E-TV, Dar es Salaam, akieleza pia utendaji wake alipokuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.



























0 Comments