Na fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam
Shirika la Sense International imelipongeza Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania nchini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na shirika hilo katika kukuza uchumi wa nchi na kusaidia kuwaunga mkono watu wenye ulemavu na kuliwezesha kukamilisha waliyoyakusudia ikiwemo kuimarisha maisha ya watu wenye ulemavu.
Kauli hiyo,imetolewa jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la kimataifa la Sense Tanzania, Naomi Lugoe wakati walipokuwa wakitoa ripoti ya tathmini ya mafanikio na changamoto za mradi wa "wezesha vijana" wenye lengo la kuwezesha vijana, kuboresha maisha na Ushiriki katika jamii kwa watu wenye uziwikutoona.
"Mpaka sasa Shirika hili ndani ya miaka mitatu kupitia mradi wa wezesha vijana tumeweza kufikia mikoa 13 na Wilaya 24 ikiwemo Dar es Salaam (Ilala), Kilimanjaro (Moshi), Mara (Tarime), Mara (Tarime), Kagera (Muleba), Morogoro (Ifakara) ambapo imewafikia vijana 36 na kuwapa mafunzo ya ujasiri amali pamoja na mitaji ya biashara"amesema Naomi.
Aidha, amesema kati ya vijana hao hao wote walifanya vizuri katika biashara zao walijitahidi na kuhakikisha biashara zao zinakua na kusimama imara, katika kujikimu mitaji binafsi pamoja na kusaidia familia kwa namna ambapo mradi huo umefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kuimarisha maisha ya uziwikutoona.
Hata hivyo, amesema licha mafanikio makubwa waliyoyapata vijana hao lakini pia wamekuwa na changamoto kubwa ya kukosa wafadhili wa kuwawesha kwani wanawaona hawawezi kufanya jambo kutokana na hali waliyonayo, hivyo wamewaomba wadau na kuwasaidia vijana hao kwa kuwawezesha kupitia miradi ama mitaji Ili waweze kujikimu kimaisha na watokane na haliya utegemezi mkubwa ndani ya familia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha viziwi wasioona Tanzania, David Kisaka amelishukuru Shirika la sense international Tanzania Kwa kushirikiana nao bega kwa bega na kutatua changamoto zinazowakabili kupitia mradi wa wezesha vijana huku akiiomba serikali na jamii Kwa ujumla kuishirikisha kundi hilo katika mambo mbalimbali ya maendeleo kuanzia ngazi za chini.
Amesema kuwa jamii imekuwa ikiwachukulia viziwi wasioona kama watu wenye matatizo ya akili jambo ambalo siyo la ukweli hivyo Kuna haja pia ya kutambuliwa rasmi hata kwenye mikopo ya asilimia 2 inatotolewa na halmashauri Kwa watu wenye ulemavu wa kutosikia na kutoona kwani kundi hilo limekuwa halipewi kipaumbele kutokana na changamoto za kimawasiliano tofauti na walemavu wengine.
Naye, Mzazi wa Husein Samata ambae ana changamoto hiyo amelishukuru Shirika hilo Kwa kuwawesha vijana kuweza kujisaidia katika kuendesha maisha yao licha ya kukutana na changamoto ya watu wanaowapa biashara zao kuzisimamia kutowapelekea pesa kwa ajili kujikimu.
"Huu mradi umetusaidia sana, mtoto wangu amewezeshwa kupata bajaji kupitia mkopo wa asilimia 2 inayotolewa na Halmashauri lakini changamoto inakuja kwa mtu ambae amepewa hiyo bajaji,afanyie kwazi haleti pesa Kwa wakati na tukienda kuifanyia marekebisho bado tunahitajika kutoa pesa na bado tunahitaji kulipa marekesho"amesema mzazi wa Samata.









0 Comments