Mwalimu mkuu wa shule ya Maria Margareth Retus Theophilo akizungumza katika mahafali hayo.
Mkurugenzi wa kampuni ya R-Gi na mjumbe wa mkutano mkuu Taifa (CCM)Prosper Tesha amechangia shule ya msingi Maria Margareth Matofali 5000,Mifuko ya Saruji 100 na Mchanga lori 3 katika harambe iliyolenga kutatua changamoto ya ukosefu wa uzio wa shule hiyo
Tesha aliongoza harambee hiyo alipokuwa mgeni rasmi katika mahafali ya kumi katika shule hiyo ambapo aliwataka wazazi na wadau wa elimu kuchangia shule hiyo ili kuhakikisha kuna kuwepo na uzio imara,ujenzi wa mabweni sanjari na uwepo wa chumba cha kompyuta ili wanafunzi wapate taaluma ya Teknolojia ya habari na mawasiliano(Tehama)
"Wazazi tunawajibu mkubwa wa kuhakikisha watoto wetu wapo salama wawapo shuleni hivyo basi lazima kuwepo na uzio imara unaoweza kuwalinda katika mazingira ya Shule "alisema Tesha
Aidha aliikumbusha jamii kupeleka watoto wa kike na wa kiume shule bila kujali jinsia zao
"Watoto wa kike wakipewa elimu wanaweza kufanya mambo makubwa sana katika jamii,tuondoke na utamaduni ambao umeshapitwa na wakati"alisema Tesha
Akitolea mfano, faida ya kumsomesha mtoto wa kike ni pamoja na kupata Viongozi mbalimbali kama alivyo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan,Spika wa Bunge la Tanzania Tulia Ackson, Mawaziri na Viongozi wakubwa kwenye Taasisi mbalimbali
Awali Mkurugenzi wa shule Bibiana Massawe akizungumza katika mahafali ya kumi shuleni hapo alisema kuwa Wazazi Walezi na Walimu kuweka kipaumbele katika kutoa malezi bora kwa watoto wadogo
"Tuanze kuweka nguvu kubwa katika kujenga msingi imara wa tabia na maadili yanayokubalika katika jamii zetu ili kuleta ustawi na maendeleo endelevu "alisema Bibiana
Pia alimshkuru Mgeni rasmi kwa kuweza kuchangia shule hiyo huku akiwataka wazazi na walezi kuendelea kulipa ada kwa wakati ili kukabiliana na changamoto zinazoikabili shule hiyo
Naye mwalimu mkuu Retus Theophilo alisema shule hiyo ilianzishwa mwaka 2009 ikiwa na wanafunzi 9 na walimu 4 hadi sasa jumla ya wanafunzi 179 na walimu12
Alisema changamoto kubwa inayoikabili shule hiyo ni pamoja na ukosefu wa uzio imara hivyo kutumia nguvu kubwa katika kuweka ulinzi wa wanafunzi na mali za shule











0 Comments