Mariam Hassan Mkali aibuka kidedea katika kinyang'anyiro cha kugombea Uenyekiti wa UWT Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani kwa kupata kura 340 Kati ya kura 641 sawa na ushindi wa Asilimia 52. 87 na kumshinda Mwenyekiti wa UWT Wilaya hiyo Rukia Masenga.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi mkuu wa jumuiya ya Wazazi Wilaya ya Bagamoyo Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi mkuu CCM na jumuiya zake ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainab Abdallah alisema aliyemfuatia ni Rukia Masenga alipata kura 273 sawa na Asilimia 42.45 huku Latifa Mwinyijuma akipata kura 28 sawa na Asilimia 4.35.
Matokeo hayo yaliyotangazwa saa 9:10 usiku Msimamizi Mkuu huyo wa Uchaguzi wa CCM Wilaya ya Bagamoyo huku akiwa viongozi mbalimbali wa CCM na viongozi wa Dini Zainab alisema ili kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa huru na wa haki ilimbidi yeye mwenyewe kwa mkono wake ashiriki kuhesabu kura moja baada ya nyingine tangu saa 11 jioni hadi muda huo.
"Kwasababu uchaguzi huo ulikuwa unatiliwa mashaka sana hivyo ilibidi kuhesabu kwa umakini mkubwa kura moja baada ya nyingine tena tumehesabu wote kura moja baada ya nyingine kuanzia nafasi ya Mwenyekiti mpaka kumalizia nafasi ya Baraza" alisema.
"Tumefanya mambo kwa uwazi na tumelazimika kuchelewa kwasababu hatukutaka hii kazi ifanywe na mtu mwingine isipokuwa Mimi Msimamizi Mkuu na Msimamizi msaidizi na wote walioingia kwenye chumba cha kuhesabu kura wamesaini kuridhika na matokeo haya"
Aidha Kamisaa huyo wa CCM aliwashukuru Wagombea wote walioshiriki uchaguzi huo sambamba na timu yote ya walioingia katika chumba cha kuhesabu kura kwa ushirikiano waluompa kufanikisha zoezi hilo la kupata viongozi wapya wa jumuhiya ya UWT Wilaya ya Bagamoyo.






0 Comments