Header Ads Widget

WALIOOMBA NAFASI ZA MAKARANI NA WASIMAMIZI SENSA WATAKIWA KUWA NA SUBIRA


Na Elizabeth Ntambala, MatukioDaimaAPP,

Rukwa 

 Wananchi wote walio omba nafasi za kuwa makarani na wasimamizi wa maudhui na maofisa Tehama wametakiwa kuwa na subira kuhusu kutangazwa kwa majina ya watahiniwa watakao shiriki kwenye usaili wa nafasi husika kwenye utekelezaji wa Sensa.


Wito huo umetolewa na kamisa wa Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 Anne Makinda alipo Kutana na kamati ya sensa ya mkoa wa Rukwa ikiwa pamoja na wadau wa Maendeleo wa mkoa wa Rukwa.


Makinda amesema sensa ina ratiba yake ambayo inatambulika kimataifa na hivyo kila kitu kitafanyika kwa wakati.


Kuna watu Wananung'unika kwanini hatutoi majina ya walio chaguliwa kuwa makarani na wasimamizi wa sensa.


Amesema kwa sasa Mafunzo ya wakufunzi ambao watafundisha makarani wa sensa ndio yanaendelea na yakikamilika yatafuata mafunzo ya makarani na wasimamizi wa maudhui.


Sensa ya watu na makazi itafanyika tarehe 23 Agost 2022 Sensa kwa maendeleo jiandae kuhesabiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI