Wananchi mkoani Kilimanjaro wametakiwa kujitokeza katika kuchangia damu ili kuwasaidia watu wenye uhitaji Kama ,akina mama wanaojifungu, waliopata ajali na watoto .
Wito huo umetolewa na Meneja wa kituo cha damu salama Kanda ya Kaskazini Dr. Edson Mollel wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi za Kanda za uchagiaji damu Zilizopo wilaya ya Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Aidha amesema katika Kilele cha maadhimisho ya siku ya wachangia damu salama Duniani kituo cha ukusanyaji wa damu salama Kanda ya Kaskazini kimekusanya Unit za damu 1,523 kati ya unit 1,076 ambazo walipaswa kukusanya ikiwa ni sehemu ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wachangia damu Duniani.
Wakati huo huo amesema kwa kanda ya kaskakasi yapo makundi mbalimbali yanayohitaji damu hivyo wananchi wanapojitolea damu itawasaidia kuokoa maisha Yao.
Kwa upande wa wananchi waliojitokeza katika kuchangia damu wameeleza juu ya umuhimu na faida za kuchangia damu .
Hata hivyo Siku ya uchagiaji damu kitaifa yameadhimishwa Leo mkoani songwe ambapo Kauli mbiu ni "Kuchangia damu ni kitendo cha mshikamano tushirikiane kuokoa maisha".







0 Comments