Dar
es Salaam; Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu Wizara ya Maliasili
na Utalii, Prisca Lwangili amewaasa wahifadhi wa misitu nchini kujenga
umoja, mshikamano na kupendana kazini ili waje kuwa na mwisho
uliotukuka.
Lwangili
ameyasema hayo Juni 10, 2022 kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na utalii Dkt Francis Michael (mgeni rasmi) wakati wa hafla ya
kuwaaga wahifadhi misitu wastaafu 61 wa Wakala wa Huduma za Misitu
Tanzania – TFS katika Jengo la Mkuki, Wilaya ya Temeke jijini Dar es
Salaam.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Lwangili amesema, ni heshima kubwa kuwaaga wenzao hao
ambao wamefikia kikomo cha utumishi wao TFS baada ya kuitumikia kwa
miaka mingi huku wakiacha alama ya utumishi uliotukuka unaoifanya TFS
kuonekana inavyoonekana hivi leo.
“Nikiwatazama
wastafu hawa naona bado wana nguvu na afya njema, hawa watu wana ujuzi
na wamefanya TFS kwa miaka 11 ya uhai wake na tunaona matokeo mazuri
walioacha, naamini kuna kanzu data yao watumieni watu hawa,
“mimi
kabla ya kuwa Wizara hii nilikuwa utumishi, TFS ni moja kati ya wakala
zinazofanya vizuri sana, tuna Wakala 27 zilizoanzishwa kufanya Serikali
iongeze mapato, kuna nyingine zinasuasua lakini TFS mko vizuri sana hii
maana yake kila mmoja wenu ameshiriki kuifanya TFS hii, na si Kamishna
wa Uhifadhi pekee, hongereni kwa hili,” anasema Lwangili.
Aidha,
Lwangili ametoa wito kwa wastaafu hao wakirudi uraiani kuendelea kuwa
mabarozi wazuri wa uhifadhi na kuendelea kushirikiana na jamii huku
akiwaasa wahifadhi wanaobaki kutambua kuwa kuanza ajira maana yake kuna
hitimisho la ajira, na hivyo wajipange.
Lwangili
anawaasa watumishi waliopo makazini kufanya kazi kwa umoja, mshikamano
na upendo kwa kile alichosema “ukimpenda mwenzako huwezi kumpiga
majungu, huwezi kumuonea wivu zaidi utajenga ukaribu naye ili kile
unachokiona kwake halafu kinakupa wivu ujifunze na wewe kikusaidie, na
kila mmoja anapokuwa yuko vizuri kwenye eneo fulani, tunatengeneza
taasisi yenye mshikamano na upendo na hivyo manung’uniko yatapungua.”
Kwa
upande wake, Kamishna wa Uhifadhi – TFS Prof. Dos Santos Silayo
amewahakikishia wahifadhi wastaafu hao kuwa TFS itaendelea kushirikiana
nao katika masuala mbalimbali pale itakapobidi licha ya kuwa wamemaliza
muda wao wa kazi.
“Napenda kuwapongeza kwa utumishi
wenu uliotukuka hadi kufikia siku ya leo, nipende kuwahakikishia kuwa
sisi mnaotuacha kazini tunaamani, mmetuachia misingi mizuri na
tutaendelea kuhakikisha taasisi hii inafikia malengo iliyokusudia, ,”
alisema Prof. Dos Santos Silayo.
Mhifadhi misitu
mkuu mstaafu Valentino Msusa anasema ni mstaafu aliyestaafu kwa heshima
pekee ndio hufanyiwa sherehe za kuagwa kiheshima na kuwataka wahifadhi
waliobaki kuzingatia sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya Serikali
na kumuomba Mungu ili wawe na mwisho mwema.
Wahifadhi misitu wastaafu walioagwa ni wale waliostaafu mwaka huu wa fedha 2021/2022.

























0 Comments