Header Ads Widget

NBS YAWANOA WAANDISHI WA MITANDAONI NCHINI JUU YA SENSA YA WATU NA MAKAZI

 


Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa mafunzo ya kuwajengea uelewa waandishi wa habari zaidi ya 30 kutoka vyombo vya habari vya mitandaoni kutoka mikoa mbalimbali nchini kuhusu zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.


Mafunzo hayo ya siku mbili yameanza Jumanne Juni 14, 2022 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Mkwawa mkoani Iringa ambapo NBS inaendelea kutoa mafunzo ya aina hiyo pia kwa wadau mbalimbali watakaosaidia kufanikisha zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kufanyika Agosti 23, 2022.

Akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo hayo, Mtaalamu wa Habari na Mawasiliano kutoka NBS, Said Ameir amesema waandishi wa habar/ vyombo vya habari ni miongoni mwa wadau muhimu katika kuhamasisha jamii kushiriki zoezi la Sensa.

Amesema maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi mwaka huu 2022 yako vizuri na kwamba matarajio ni kukamilika mapema na kwa wakati kutokana na matumizi ya teknolojia ya kisasa inayotumika kukusanyia takwimu ambapo maswali yote muhimu yatakuwa pia kwenye vishikwambi na hivyo kuwarahisishia makarani kujaza taarifa.

Amesema zoezi la Sensa nchini hufanyika kila baada ya miaka 10 na lina manufaa makubwa kwa jamii kwani husaidia Serikali kupata taarifa na takwimu muhimu kwa ajili ya mipango ya maendeleo na hivyo kuwahimiza wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani wakati wa zoezi hilo.

Kwa upande wake Mratibu wa Jukwaa la Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) ambaye pia ni Mkurugenzi Gilly Bonny TV amesema mafunzo hayo ni muhimu na yatawasaidia waandishi wa habari wa mitandaoni kuelimisha na kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ili makarani watakapokuwa wanapita kwenye kaya zao wawape ushirikiano na wasiwe na hofu ya kujibu maswali watakayoulizwa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI