Na Amon Mtega, Matukio DaimaAPP,Songea.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Ruvuma Tito Mbilinyi(MWILAMBA)amempongeza mheshimiwa Rais wa Jumuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suhulu Hassan kwa kuzitambua changamoto ambazo zilizokuwa zikiwakabili Wafanyabiashara na kupelekea baadhi yao kuzifunga biashara zao.
Mbilinyi amezitoa pongezi hizo baada ya mheshimiwa Rais kutoa maelekezo kadha kwenye sekta inayohusika na wafanyabiashara kuona namna ya kuwaondolea kero ambazo zimekuwa zikiwakabili hasa katika maeneo ya ulipaji Kodi.
Mwenyekiti huyo amesema kuwa katika kipindi cha nyuma wafanyabiashara wamekuwa wakilalamikia kodi zimekuwa zipigiwa hesabu za juu tofauti na biashara inayofanywa jambo ambalo limewafanya baadhi ya wafanyabiashara hasa wenye mitaji midogo kufunga biashara zao na wengine kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa kwa baadhi ya maafisa wasiyo na uzalendo.
"Nampongeza sana Rais wetu Samia Suhulu Hassan kwa kuibua suala hili lilikuwa ni kilio kwa wafanyabiashara sasa tunaamini hakuna mfanyabiara atakayekwepa kulipa kodi "amesema mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Ruvuma Tito Mbilinyi.
Akitolea mfano amesema kuwa kumekuwa na mlundikano wa kodi hata kwenye Halmashauri ambazo nazenyewe zingeweza kuangaliwa namna ya kuziweka sawa ili kumlinda mfanyabiara mdogo aweze kumudu kulipa kodi hizo.
Aidha mwenyekiti huyo amezungumzia baadhi ya changamoto ambazo wanakutana nazo hasa wafanyabiashara wa Mkoa wa Ruvuma kuwa watu wa makadilio ya mahesabu wapo wachache na kuwa mkoani hapo hawazidi wawili jambo ambalo hupelekea baadhi ya wafanyabiashara kuwaomba watu wa makadilio wasiyokuwa na sifa na mwisho wa siku inawaletea shida pindi wanapotaka kulipa kodi.
Kufuatia changamoto hiyo kukosa watu wa makadilio amekiomba chama cha wahasibu kuona umuhimu wa namna ya kuwaongeza wataalamu wa makadilio kwenye Mkoa huo .
Mwisho.






0 Comments