Header Ads Widget

JAMII YA KIFUGAJI WILAYANI LONGIDO YATAKIWA KUANZA MIKAKATI YA UPATIKANAJI WA CHAKULA SHULENI.

 



 Teddy Kilanga MATUKIODAIMA APP Arusha



Mkurugenzi wa shirika la World vision Tanzania,Gilbert Kamanga ameitaka jamii ya kifugaji wilayani Longido kuweka mikakati ya upatikanaji wa chakula shuleni kwa lengo la kuhimarisha afya za wanafunzi pamoja na kuongeza ufauli wa masomo.



Akizungumza katika hafla ya kukabidhi chakula katika Tarafa ya Ketumbeine wilayani Longido,Kamanga alisema sasa hivi wanatoa chakula kupitia mradi wa Ketumbeine AP kutokana na janga la njaa liliosababishwa na ukame kwa kipindi kilichopita.



"Ni vyema wazazi mkaanza mikakati sasa hivi ya upatikanaji wa chakula shuleni ili mradi huu utakapoisha watoto waendelee kupatiwa chakula shuleni kwani inasaidia kupunguza idadi ya utoro shuleni,"alisema Kamanga na kuongeza kuwa wanafunzi kwa sasa afya zao zimehimarika tofauti na huko nyuma.



Kamanga alisema chakula walichotoa ni takribani tani 117 za mahindi na 37 za maharage pamoja na mafuta ya kupikia ndoo 307  zenye ujazo wa lita 20 kila moja vyenye thamani ya sh.milioni 227.3 ambapo wanufaika ni watoto 10,272 kutoka shule za msingi 24.



Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ketumbeine Felix Mungaya alisema utoro wa wanafunzi umepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na uwepo wa chakula shuleni kwani imewaletalea tija hata katika ufundishaji na kuongeza ufaulu wa wanafunzi.



"Nikiri kupitia msaada huu wa chakula shuleni umeleta tija kwetu katika ufundishaji madarasani wanafunzi hawasinzii kwa katika kipindi cha nyumba walikuwa wanachoka kwa njaa hali iliyokuwa inapelekea wanatoroka shule lakini sasa hivi watoto wenyewe wanang'ang'ania kubaki shule hasa wale wa kutwa,"alisema Mwalimu Mungaya.



Mwanafunzi wa shule ya msingi Ketumbeine Kaleb Israel alilishukuru shirika la World vision Tanzania kwa kuwaboreshea miundombinu ya shule ikiwemo matundu manne ya vyoo na bafu nne,kisima kimoja cha kuhifadhia maji,bweni moja la wavulana lenye uwezo wa wanafunzi 72,Vitanda doube deka 50 na magodoro 100,"alisema .



Aliongeza kuwa vitu vingine ni pamoja na Simtank mbili zenye ujazo wa lita 5000 kwa kila moja pamoja na madumu matano kwa ajili ya kunawia mikono kwa lengi la kujikinga na maradhi mbalimbali ya mlipuko.



Pia alisema shirika la World vision Tanzania limekuwa likiwasaidia kuwapa mafunzo ya kujitambua ili kuepuka mimba za utotoni,madhara ya ukeketaji pamoja na haki za watoto.



Mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Longido,Boniphace Lugola alisema shirika hilo limkuwa msaada katika jamii hiyo ya kifugaji  pamoja na kufufua maendeleo katika Tarafa hiyo lengo ni kuinua uchumi wa wananchi mmoja mmoja na hata wilaya kwa ujuma.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI