Header Ads Widget

BMF KUFANYA MDAHALO KUMBUKUMBU YA HAYATI BENJAMIN MKAPA.

 


Na Fatma Ally Matukio Daima APP Dar es Salaam


Taasisi ya Benjamin Mkapa Foundation (BMF) inatarajia kufanya mdahalo wa siku mbili wa kumbukumbu ya aliyekuwa Rais wa awamu ya  tatu Benjamin William Mkapa ambapo utashirikisha jopo la wadau watakao chambua kwa undani umuhimu wa Biashara ama uwekezaji wa pamoja katika kuinua afya na ustawi wa kila mmoja.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya BMF, Dkt  Ellen Senkoro amesema kuwa mdahalo huo utafanyika Julai 13 na 14 katika Hotel ya Golden Tulip Visiwani Zanzibar, ambapo utashirikisha wageni takriban 500.


Amesema kuwa, katika mdahalo huo kutakuwa na mada mbili ambazo zitajadiliwa ikiwa ni  kuongeza kasi katika mikakati ya mabadiliko katika mifumo ya afya Tanzania kupitia biashara ushirika pamoja na ubunifu katika miradi na mikakati ya ushirikiano kati ya Serikali, Taasisi za umma na za binafsi katika kuleta huduma ya afya kwa wote.


Hata hivyo, amesema, kupitia mdahalo huo washiriki watapata fursa ya kuskia juhudi za mashirikiano ya Serikali ya Tanzania Bara na Visiwani, Sekta binafsi pamoja na wadau wa maendeleo pamoja na juhudi zilizochagizwa na Taasisi ya BMF, katika kuimarisha mifumo ya afya kwa lengo la kuhakikisha kila mtu popote alipo anapata huduma bora za afya.


Aidha, amesema kuwa, Mkutano huo wa siku mbili  utafufunguliwa na Makamo wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, huku ukifungwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ambapo mwenyeji wa Mkutano huo akiwa ni Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Hussein Ali Mwinyi.


Hata hivyo, amesema viongozi mbalimbali watashiriki katika mdahalo huo wakiwemo viongozi wakuu wa Serikali, Marais na viongozi wastaafu kutoka Tanzania Bara na Visiwani , mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini Tanzania,wakuu wa mashirika ya kimataifa pamoja na wakuu wa mataifa mbalimbali za Sekta binafsi na umma.


Kwa upande wake, Meneja Tathimini na ufuatiliaji wa Miradi BMF, Rahma Musoke amesema miongoni mwa kazi zinazofanywa na Taasisi hiyo katika kukuza miradi ni pamoja na kuongeza wataalamu wa afya ndani ya jamii .


Aidha amesema pia wamejenga nyumba za watumishi 482 hususani katika maeneo magumu ambayo hayafikiki pamoja na kuboresha vituo 537, huku asilimia 80 ya watumishi wa huduma za afya wameajiriwa Serikali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI