MKUU wa mkoa wa Iringa Queen Sendiga amekagua miradi ya barabara Katika Halmashauri ya wilaya Iringa ,barabara zinazojengwa Kwa fedha za tozo za faida ya nyongeza ya tozo za mafuta.
Akikagua leo ujenzi wa kiwango Cha changarawe wa barabara ya Ikengeza ,Mkungugu -Nyang'oro yenye urefu wa Kilometa 10 , Sendiga amesema kukamilika Kwa barabara hiyo ni ukombozi mkubwa Kwa wananchi wakulima wa mpunga pia itasaidia kukuza uchumi Kwa Taifa .
Sendiga amepongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kutoa fedha Kwa ajili ya Utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kimaendeleo ndani ya mkoa wa Iringa na kuagiza wananchi kutunza miradi inayojengwa .
Meneja wa wakala wa barabara mijini na Vijijini (TARURA) Halmashauri ya Iringa Barnabas Jabiri amesema ujenzi wa barabara hiyo utakaogharimu zaidi ya Milioni 137 unatekelezwa na mkandarasi mzalendo Boimanda wa Mafinga mkoani Iringa .
Huku wananchi wa Kijiji Cha Ilambilole wakipongeza ujenzi wa barabara hiyo kuwa na ukombozi mkubwa kwao
0 Comments