Header Ads Widget

RC MWANZA ASIMAMISHA MIKOPO KWENYE HALMASHAURI


Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel amesimamisha utoaji wa mikopo ya Halmashauri kwa Halmashauri nane zilizopo katika mkoa huo kwa muda wa mwezi mmoja ili kupisha uchunguzi wa kamati maalum kuchunguza namna fedha hizo zilivyotolewa na kutumika ikiwemo na kuhakikisha vikundi vinavyochukua mikopo hiyo vinapata elimu.


Akizungumza na waandishi wa habari Rc Gabriel amesema ametoa kauli hiyo baada ya kubaini upotevu wa zaidi ya shilingi bilioni 4 zilizotolewa kwa vikundi ndani ya miaka mitatu kutorejeshwa hadi sasa.


katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa wa Mwanza akawataka watumishi wa umma na waajiriwa wote waliojifanya wajasirimali na kuchukua mikopo hiyo kuacha tabia hiyo mara moja ikiwemo na kurejesha fedha walizochukua.


Aidha ameiagiza TAKUKURU kufatilia ubadhilifu wa fedha hizo na kuwakamata watakaobanika na ubadhilifu  huo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI