Na Teddy Kilnaga Matukio DaimaAPP,Arusha
Kamati ya viongozi na wataalamu juu ya mgogoro wa Ardhi ya Tarafa ya Ngorongoro, Sale na Loliondo umemaliza mchakato wa kukusanya mapendekezo kwa wananchi umefikia tamati kwa ajili ya kuwasilisha serikalini.
Akizungumza Mwenyekiti wa kamati hiyo,Metui Sheudo alisema mchakato huo wa mapendekezo uliotumia takribani wiki mbili umefikia tamati kwa ajili ya kuwasilisha katika ofisi ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
"Ukusanyaji wa maoni haya kutoka kwa wananchi ni kwaajili ya kutatua migigoro ya ardhi katika eneo lenye kilometa za mraba1500 bila kuathiri pande zote mbili,"alisema.
Metui alisema hatua hiyo ilifuata baada ya mchakato wa kuwashirikisha wananchi na makundi mbalimbali katika jamii kuwa hafifu katika kutatua mgogoro huo.
Aidha aliongeza kuwa kutokana na hilo waliona kutumia njia hiyo ambayo itasaidia kupata mapendekezo kwa jamii katika kufikia wahusika na umma wa wahusika kwa ujumla kupitia viongozi wao.
Hata hivyo alisema wanaiomba serikali kupitia Waziri Mkuu kukemea vitendo vya ukamataji holela wa viongozi wakiwemi madiwani wanaosimama kutetea haki za jamii hiyo.
Alisisitiza kuwa wanaishauri serikali kutotumia mchakato wa watu kuhama kama silaha ya kuwagawa jamii ya wanangorongoro.
"Tunaiomba serikali kuzuia propaganda zozote dhidi ya wananchi wa Ngorongoro hasa jamii ya kimasai na kusitisha michakato yote inayoendelea ili kutoa nafasi ya kusikiliza maoni yaliyotolewa na jamii ili kutoa fursa ya utatuzi mgogoro huu kwa amani,"alisema Mwenyekiti huyo.
0 Comments