Header Ads Widget

JIJI LA MWANZA LINATARAJIA KUTOA KIASI CHA TSH MILIONI 80 UJENZI MADARASA

 


Halmashauri ya jiji la mwanza inatarajia kutoa kiasi cha shilingi  milion 80 zitakazokutumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa 6 kwenye shule ya msingi mabatini A, kutokana na vyumba vya sasa kuwa na uchakavu mkubwa na kuanza kubomoka huku mengine kuweka nyufa jambo mbalo linahatarisha usalama wa wanafunzi hao na kusababisha msongamano mkubwa kwenye madarasa.   

    Akizungumza mara baada ya ukaguzi wa vyumba   vya madarasa shuleni hapo mstahiki meya wa jiji la mwanza Constantine sima amesema halmashauri hiyo licha ya kuwa na mpango wa  ukarabati wa shule zote kongwe za msingi   katika jiji la mwanza lakini kwa sasa kipaumbele ni  kuanza mashule hyo ambayo madarasa yake yana halimbaya.

    


  Naye mwalimu mkuu wa  shule hyo amesema jitihada za haraka zinahitajika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa ili kuondoa msongamano .

     Kwa upande wao wanafunzi wa shule hyo wamesema wanalazimika kukaa wanafunzi 160 darasani hali ambayo inawafanya wabanane nakushindwa kujisomea vizuri.


  Shule ya msingi mabatini A ilianzishwa mwaka 1978, na ina wanafunzi zaidi ya elfu moja huku ikiwa na uhaba wa vyumba vya madarasa 20.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI