Header Ads Widget

PUMZIKA KWA AMANI PROFESA HONEST NGOWI

 

Na Victor Tesha

Siku ya leo majira ya saa 3 asubuhi, nilipokea taarifa mbaya sana za kuondokewa gafla na mwalimu wetu wa uchumi Prof Honest Ngowi akiwa na dereva wake maeneo ya Mlandizi Dar es salaam, Chanzo cha kifo chake ni ajali mbaya ya gari.

Nilimfahamu professor Ngowi mwaka 2007- 2009 chuoni Mzumbe nikiwa mwanafunzi wa masters - MBA. Yeye alikuwa anatufundisha  Managerial Economics. Siku ya kwanza naingia chuoni nilimfwata nikamwambia sijawahi kusoma Economics A - Level wala First Degree ila ni somo nalipenda na ningependa ku opt masomo mengi zaidi ya uchumi. Aliniangalia kwa upole na tabasamu akasema _I will make it simple for you_ . Kweli alitenga muda wake kunifundisha alinipa “material” ya ziada. Alipokea simu muda wote wanafunzi tulipokuwa tunamtafuta na alifanya kwa furaha. Kwa kifupi alipenda kuutoa elimu bila kinyongo, hata kama amechoka alitufundisha hata kwa kusimama kwenye korido. Hakusifika kwa kufelisha makusudi (kuwapa wanafunzi supplementaries ) alifundisha kwa ustadi mkubwa uliosababisha hata mtu mwenye IQ ndogo kumwelewa kupenda somo lake na kufaulu. 

_Professor Ngowi naweza kusema ulitushika mikono yetu, ukafunguwa akili zetu, na ukagusa  mioyo yetu. Maelfu ya wanafunzi waliopita katika mikono yako wanakulilia, taifa linahuzunika_

Huwa tunazungumza mara kwa mara kwa simu na sometimes kuonana lakini  last week nilimpigia simu akapokea kwa uchangamfu mkubwa sana akaniambia pita ofisini Tesha… kwa utani akasema “we make things simple” nikacheka nikamwabia bila shaka nitakuja. Nilifika na tulikaa kwa masaa kadhaa tulicheka sana. Tulijadili mambo makuu 2 la kwanza ni Diplomasia ya uchumi wa Africa Mashariki ukizingatia DRC nayo inaingia kwenye jumuiya yetu na pili michango ya waajiriwa wa Kitanzania kiutendaji katika taasisi za Africa mashariki, je tunaajirika? Na kama hatuajiriki nini kifanyike? Basi tulihitimisha mkutano wetu nikamwomba anisaide ku “proofread” article yangu kwa furaha kabisa akakubali nikamtumia kwa email. Wakati nataka kuondoka alinipa zawadi ya vitabu 2 alivyoandika yeye vya uchumi nikajisomee, nilifurahi sana na nilipiga naye picha ya ukumbusho na asante. Jana akani text naomba nitumie email nikurushie kazi yako tayari.

TUNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA MAISHA YA MPENDWA WETU PROF NGOWI?

1:  Ukipewa talanta na Mungu share na wenzio kwa upendo na furaha usiitumie kama fimbo kuadhibu watu wa Mungu. Alitoa elimu ya uchumi mara nyingi bure kabisa bila kuchoka. Sote tuliona jinsi vyombo vya habari vilivyokuwa vinamhoji kila mara endapo kuna sintofahamu katika mambo kadhaa. 

2: Maisha ni mafupi sana, ukiwa unatoka nyumbani kumbatia mkeo, wazazi na watoto wako waambie unawapenda na msali walau sala fupi, wabusu (kiss them) waambie unawapenda. Inaweza kuwa mara yako ya mwisho kuwaona, labda unawaaga. 

3: Kuwa mtu wa kutoa huduma katika eneo la kazi, Prof Ngowi alisifika kwa open door policy alimwona mtu yeyote alimsikiliza yeyote bila kujali ana nini au nyadhifa gani? Wanafunzi walijaa ofisini kwake na hakuzuia mtu kumwona. 

4: Prof Ngowi alijiajiri kwenye kilimo cha kufuga na kulima, alitoa ajira kwa vijana wengi alikuwa na online TV yake ambayo ilituelimisha na kuajiri pia. 

5: Make things simple, kokote ulipo rahisisha maisha ya watu waliokuzunguka, maisha yenyewe haya ni magumu tayari. Ukiwabania watu ili wewe ufanikiwe still utakufa na utaacha kila kitu. Prof Ngowi alipenda kuniambia I will make it simpe for you… make life easy to others. 

6: Pokea ushauri hata kama wewe una elimu kubwa au ni kiongozi mkubwa, juzi nikiwa na prof ofisini kwake alinionyesha ujumbe niliomwandikia mwaka 2015 nikimshauri aanzishe online TV ili kuwafikia watu wengi zaidi, akacheka akaniambia siunaona inafanya vizuri? Akasema asante Tesha nilikusikiliza sasa nataka niweke material mengi zaidi. 

Itaendelea……

USISAHAU KUPATA BURE APP YA MATUKIO DAIMA KUPITIA GOOGLE PLAY STORE

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI