Header Ads Widget

KAMPUNI YA FOXES TRECK NI MFANO WA KUIGWA YAJENGA ZAHANATI YA IGODA , VIONGOZI WAPONGEZA


UONGOZI  wa kijiji cha Igoda  kata ya  Luhunga  wilaya ya  Mufindi  mkoani  Iringa  umepongeza jitihada  kubwa  zinazofanywa na kampuni ya Foxes Treck  kupitia  taasisi yake  ya Foxes Community and  Wildlife conservation (FCWC) kwa  kujitolea  zaidi ya  Tsh milioni 100 kujenga  wodi  ya  wazazi na  Zahanati .


Akizungumza  jana  kijijini hapo mara baada ya mfadhili  huyo  kutembelea  kuona maendeleo ya  ujenzi   huo ,afisa  mtendaji  wa  kijiji  cha Igoda  Laines Sanga  alisema  kuwa  kampuni  ya  Foxes  Treck  ambao  ni  wawezekezaji wazawa katika  kijiji  hicho imeendelea  kusaidia shughuli  mbali mbali  za  kimaendeleo zikiwemo za  ujenzi  wa miradi ya  elimu ,afya na miundo  mbinu ya  barabara  ndani ya  eneo lao.




Hivyo  alisema  wao kama  kijiji  wanajivunia   kuwa na mwekezaji  huyo ndani ya  eneo  lao kwani  pamoja na kufanya  shughuli  zake  za  uwekezaji  ila amekuwa ni nguzo ya maendeleo ya  kijiji  hicho na vijiji vingine.


"  Tunamshukuru  sana mfadhili  wetu  Foxes Treck  kijiji  chetu  kilikuwa na changamoto ya  uhaba wa Zahanati ila  ameweza  kutujengea  pamoja na kujenga  nyumba  za watumishi kwenye  kituo  hiki  pia  wana Igoda  wanajivunia  sana  kuwa na mdau  wetu  wa  maendeleo anayetujali wananchi " alisema Sanga 



Kwa  upande  wake  muuguzi mkunga  wa  Zahanati  hiyo ya  Igoda  Bahati  Ndelwa  mbali ya  kushukuru kuwepo  kwenye  Zahanati  hiyo  ila  alisema  uwepo  wa Zanahati  hiyo  umesaidia  sana  kupunguza vifo  vya  akina mama  wanaokwenda  kujifungua  kwani  toka  afike  kituoni hapo  hakujatokea  kifo  hata  kimoja  kutokana na  huduma nzuri  inayotolewa  kwenye  Zanahati  hiyo  iliyojengwa na mfadhili  Foxes  Treck .


 Hata  hivyo  alisema  changamoto  kubwa  ni  uhaba wa  watumishi  kwenye  Zahanati  hiyo  ambayo  kwa  sasa  kuna  watumishi wawili  pekee  hivyo  ikitokea  mmoja anatatizo inamlazimu  mtumishi  mmoja  kufanya kazi  zote .


Hivyo  aliomba  serikali  kusaidia  kuongeza  idadi ya  watumishi  ili  kuboresha  zaidi   huduma katika  Zanahati  hiyo.


Meneja  wa FCWC Zilipa  Mgeni  alisema  kuwa kampuni  hiyo ya  Foxes Treck  imeendelea  kusaidia  miradi  mbali mbali  katika  kata  zote  tatu za Ihanu ,Mdabulo na  Luhunga   na kuona   vijiji vinavyozunguka  kampuni  hiyo  vinasaidia  miradi ya  kimaendeleo.



Aidha alisema  wao kama  wafanyakazi wa  kampuni ya  Foxs  Treck  wanaipongeza kampuni  hiyo  kwa  kuwa na  ushirikiano  mzuri  na  jamii  pamoja na  serikali  kwa  kujitolea   kuhudumia  jamii pasipo  mitafaruku .


Mgeni  alisema  Sanjari na  kujitolea  kusaidia  miradi ya  kimaendeleo  pia  kampuni   hiyo  imeendelea  kusaidia  watoto  wenye mazingira  magumu pamoja na Yatima  kupata  elimu jambo ambalo  limesaidia jamii  hiyo  kuwa na mfariji  mwema .


Kwa  upande  wake mkurugenzi  wa kampuni  ya  Foxes Treck  Geoff Foxes  alisema  kuwa  kuwa  kampuni yake   inatambua  umuhimu  wa  afya  bora  kwa  wananchi  wake na   hivyo ndio  sababu ya  kujitolea  kujenga  Zanahati  hiyo na nyumba  za watumishi .


Hata  hivyo alisema ili  huduma  ya  afya  iweze  kuboreshwa  zaidi ni lazima  wahudumu  wawepo  wa kutosha ambao  watasaidia  kufanya  huduma  kuwa  bora  vinginevyo  majengo pasipo  watumishi  hayatasaidia  kuwa na huduma  bora  za  afya .


Foxes  alisema  kuwa huduma  bora  za  afya  ni pamoja na  uwepo  wa  uzazi  wa  mpango na kuwa katika  Zanahati  hiyo  ameweka  chumba   cha  uzaji  wa  mpango  na  kuwa  lengo  na  kuona  jitihada  za  serikali  za  uboreshaji wa  afya  zinakwenda  sawa .


Pia  alisema  lengo la  kampuni yake  ni kuendelea  kuiunga  mkono  serikali  iliyopo madarakani   katika kuwahudumia  wananchi  wanaozunguka  kampuni  hiyo  na  kampuni yake  itaendelea  kuwa  bega kwa  bega na wananchi  pamoja na  serikali katika uchangiaji  wa  miradi ya  kimaendeleo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI