Header Ads Widget

MNUFAIKA WA AGRA IWAWA GENERAL SUPPLIES AFUNGUKA

 


WANUFAIKA  wa shirikisho la mageuzi ya kijani Afrika(AGRA) mkoani  Iringa    wamemweleza  mjumbe wa kamati ya  mipango  bodi ya  AGRA  Dkt Jakaya  Kikwete ambae ni   Rais wa awamu  ya nne  wa  Jamhuri ya muungano wa Tanzania changamoto wanazokabiliwa nazo katika  kukuza  mitaji yao .

 

Akizungumza  jana mjini Iringa  wakati  wa  ziara ya  mjumbe  huyo wa bodi ya AGRA na msafara  wake  ,Mnufaika  Emanuel  Sanga  ambae ni  msambazaji  wa Pembejeo  kutoka kampuni ya  Iwawa  General Supplies  mbali ya  kupongeza  AGRA kwa  kuwaunganisha  na wanavikundi wapatao 20 vijijini  na  sasa  wamekuwa  wakienda  vizuri  pamoja na uwepo  wa   changamoto  ambazo  wameomba  serikali kupitia wizara ya  Kilimo kushughulikia .

 

Alisema  kupitia jitihada  hizo  za  AGRA  kuwaunganisha  na  vikundi  vya  wajasiriamali  wadogo  vijijini na  elimu  mbali  mbali  ambazo  wameendelea  kuzitoa  bado  wanaomba  wizara ya  Kilimo  kuangalia  uwezekano  wa  kuwainua  zaidi   kwa  kuwapatia  mikopo  ya  kukuza  biashara  yao.

 

“ Kupitia mafunzo  yaliyotolewa na AGRA  kwa  wakulima  na  wasambazaji  wa  Pembejeo   imesaidia   wao  kuongeza  mitaji yao kupitia mkopo  wa  taasisi ya  kibenk ambao  waliomba ili  kukuza  biashara   hiyo”

 

Alisema  changamoto  ni  mitaji  midogo na hivyo  kuomba    kupatia  mikopo  yenye  riba nafuu  ili  kuwawezesha  kuongeza kasi ya  usambazaji  wa pembejeo kwa  wakulima .

 

Sanga  alisema  mikatati yake ni  kuanza  ufugaji wa ng’ombe  kama 500 na kuku  wa mayai kama 1500 ili  kupitia mradi  huo  waweze  kununua mazao  ya  wakulima kwa  ajili ya   mifugo .

 

Kwa  upande wake Dkt   Kikwete    ameamepongeza jitahada kubwa zinazofanywa na  AGRA nchini Tanzania katika kukuza kilimo na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo.

 

Dr Kikwete ambae  aliweza  kuwatembelea wachakataji wa mazao ya kilimo na wauzaji wa pembejeo na kujionea namna ambavyo wadau hao wa kilimo wamesaidia kujiongezea kipato na kutengeneza fursa nyingi za Ajira  kwa wakulima wengi na hivyo kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa sekta ya Kilimo.

 

“Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Mipango ya AGRA,tulikubaliana kwenye Bodi kwamba wajumbe tupite kukagua miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na AGRA.

 

Nimefarijika kuona miradi mingi ni mizuri na imeleta athari chanya kwa wakulima wetu na wachakataji wa mazao ya kilimo,hii itasaidia sana kukuza sekta ya kilimo na kukuza uchumi wa Nchi yetu”Alisema Dr Kikwete

 

Naibu Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde aliishukuru AGRA kwa kazi kubwa inayofanya katika kumjengea uwezo mkulima wa nchi hii na kuhakikisha kwamba zao la kilimo linaongezewa thamani jambo ambalo ndio muelekeo wa serikali na kuahidi kutoa ushirikiano kwa Taasisi hiyo ili malengo ya nchi kupitia kilimo yaweze kutimia.

 

Ziara   hiyo  mkoani  Iringa Dr Kikwete aliambatana na makamu wa Rais  wa AGRA Aggie Asimwe Konde pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI