Header Ads Widget

"CHAGUENI VIONGOZI WANAOJALI MASLAHI YA NCHI NA SIO MASLAHI BINAFSI"_ DKT. KIKWETE

 


RAIS Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Kikwete amewataka wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchagua viongozi watakaojali maslahi ya chama na siyo watakaojali maslahi binafsi.


Dk Kikwete amesema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 45 ya CCM mkoa wa Pwani ambapo kimkoa yamefanyika Chalinze wilayani Bagamoyo.


Amesema kuwa ni vema wanachama wa CCM wakatumia vizuri uchaguzi wa ndani ili kupata viongozi bora.



"Chagueni viongozi wazuri watakaotupeleka mbele msichague viongozi ambao watatanguliza maslahi yao ambao wanatafuta uongozi kwa ajili yao," amesema Kikwete.


Aidha amesema kiongozi anayetakiwa ni yule atakayetumia muda wake kukitumikia chama na si kwa ajili ya mambo yake binafsi.


Amempongeza Rais wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa uongozi wake imara na ujasiri kwani ameweza kufanya kazi nzuri ya kuwatumikia wananchi.



Naye mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Bagamoyo Abdul Sharifu amesema kuwa wameridhishwa na utekelezaji wa ilani kupitia Rais Samia Suluhu.


Sharifu amesema kuwa wilaya ya Bagamoyo imepata miradi mingi ya maendeleo ambayo inaleta manufaa kwa wananchi.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI