Baraza la halmashauri ya wilaya ya Kibaha vijijini mkoa wa Pwani limeuomba uongozi wa halmashauri hiyo kuhakikisha inasaidia upatikanaji wa fedha ili vijana watakaopata fursa ya kuendesha zoezi la anuani za makazi katika eneo hilo Sanjari na kushirikishwa katika masuala mbalimbali ya maendeleo.
Hayo yalisemwa katika kikao Cha Baraza la madiwani kuwasilisha Taarifa mbalimbali za maendeleo ya kata baada ya kuwepo na mkanganyiko wa sintofahamu namna ya kuwawezesha Vijana hao katika malipo.
Shomari omari ni diwani kata ya soga alisema zoezi Hilo ni muhimu na Vijana watakaojitokeza hawana budi kuthaminiwa ili kusaidia kupata taarifa sahihi zitakazosaidia uboreshaji katika zoezi la sensa ya watu na makazi .
Hili suala tunaomba kujua huku kwetu mwenyekiti aliulizia kuhusu malipo na aliambiwa hakuna posho kwa shughuli la zoezi Hilo hamuoni Kama litaenda ndivyo sivyo.Alisema Shomari.
Kwa upande wake MBUNGE wa Jimbo la kibaha vjiji Michael Mwakamo Alisema kumekuwa na sintofamu mitaani kuhusiana na zoezi hili la anuani za makazi,Hilo ni zoezi tangulizi kuelekea zoezi la sensa ya watu na makazi hivyo ni wajibu wetu kulifanya kwa weledi ili kufanikiwa katika shughuli zingine za maendeleo
Zoezi hili kuwakabidhi watendaji wa vijiji na kata kuwaachia kulipa Vijana hao kutokana na mapato yanayotokana na vijiji hivyo Bado ni changamoto maana Kuna baadhi ya vijiji havina mapato ya kutosha na kuwalipa Vijana hao hii hatutaweza kutoka na majibu mazuri ya zoezi hii yanayotolewa usoni lkn Lina changamoto.
"Watendaji wa vijiji hawawezi kumkabili mwenyekiti kwa maneno magumu kuwa hawana mapato ya kukidhi malipo hayo kwa vijana.
Tunaomba ofisi ya Mkurugenzi iliangalie hili kwa jicho la tofauti na kuepuka kutoa maneno yenye kufariji kuwa zoezi linaenda vizuri tuwe wakweli na ukimya ukichukukiwa kama ni sehemu ya nidhamu inachelewesha maendeleo kwa wananchi.Alisema Mwakamo.
Akijibu maswali ya madiwani mwanasheria wa halmashauri hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Grace Muhagama kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji Alisema kuwa wameshaandikia barua watendaji wa vijiji na kata wanajukumu la kuwawezesha ,chakula ,maji na posho na inategemea na Pato na Kijiji na wingi wa nyumba zilizopo katika eneo husika.
"Halmashauri ilishatoa jukumu Hilo kwa watendaji wa vijiji na kata kuwawezesha Vijana watakaofanya zoezi la anuani la makazi kwa kuhakikisha wanapewa posho isiyopungua 10000 ,maji na chakula.Alisema Muhagama.
Pia Muhagama Alisema kuwa katika zoezi hilo la makazi walianza kutambua nyumba 27,000, na viwanja havijaendelezwa kwa mujibu wa maelekezo ya mamlaka ya mji mdgo na pia wanaendelea kuzipa namba nyumba hizo na kutambua vijana watakaoshughulika na zoezi hilo la mfumo.
Halmashauri haina bajeti ya kuwalipa Vijana hao zaidi ya kutoa maelekezo kwa ngazi ya vijiji na kata na mpaka Sasa wameshapatika Vijana 102 kwa ajili ya kufanya zoezi Hilo ambapo watapewa elimu ya mafunzo.Alisema Muhagama.
0 Comments