Header Ads Widget

TRA YAPOKEA MSAADA HUU KUTOKA JICA


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo imepokea msaada wa magari matatu na boti moja ya mwendo kasi  kwa ajili ya kudhibiti magendo kutoka Shirika la Maendeleo la Japani (JICA).Mwandishi Fatma Ally MDTV Dar es Salaam


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamishna wa TRA, Alphayo Kidata amesema kuwa, lengo la msaada huo ni kuimarisha doria katika mikoa mbalimbali inayopitisha magendo ikiwemo Dar es Salaam, Kasimulo pamoja na Mkoa wa Tunduma .


Aidha, amesema kuwa, licha ya magari hayo lakini pia wamepokea boti ya mwendo kasi kwa ajili kusaidia kulinda mikapa kwa upande wa bahari ya Hindi hali itakayopelekea kuongeza ukusanyaji wa mapato, Sambamba kupokea na Unit 14 kwa ajili kudhibiti madawa ya kulevya na kulinda afya za watanzania.


Ameongeza kuwa, dhana nzima ya msaada huo ni kuhakikisha Mamlaka a mapato TRA wanapata mapato yake halali na kuzuia uvujaji wa mapato kutokana na biashara  magendo.


Aidha amelishukuru Shirika hilo kwa kutoa msaada huo ambao utasaidia kustawisha maendeleo ya watanzia na ustawi kwa ujumla.


Kwa upande wake, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Goto Shinichi amesema katika kuendeleza maendeleo ya kikanda kupitia kibiashara na ulinzi wa mipaka kwa nchi za Afrika Mashariki wamekubaliana na Japani kuanzisha mradi wa msaada wa pamoja  kwa ajili ya kulinda mipaka ya nchi hizo.


Aidha, amesema Japani imetoa dola za kimarekani Mill  3.2 kwa kununua vifaa hivyo, kwa lengo la kushirikiana kati ya JICA na TRA kwa ajili ya ulinzi wa Nchi, usalama wa mipaka pamoja na kukuza biashara za kikanda.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI