Header Ads Widget

SERIKALI IMESAINI MKATABA WA HUDUMA WA KUCHAKATA GESI ASILIA

 


Serikali ya Tanzania kupitia shirika la Maendeleo la Petroli nchini TPDC imesaidi mkataba wa huduma ya ushauri elekezi katika mradi wa kuchakata gesi asilia(LNG) na Kampuni ya Baker Botts ya nchini Uingereza ikiwa ni hatua nzuri ya mradi utakaojengwa Mkoani Lindi.Mwandishi Teddy Kilanga anaripoti kutoka Arusha 

Mradi huo unatarajia kutumia gesi kutoka katika vitalu namba 1, 2 na 4 mkoani humo na kuuzwa katika masoko ya nje ambapo gharama za mradi huu zinakadiriwa kuwa Dola za Marekani bilioni 30 sawa na takriban Sh70.5 trilioni. 

​Hata hivyo, utekelezaji wa mradi huo umekuwa ukipigwa danadana kutokana na kutokamilika kwa majadiliano baina ya wawekezaji wa mradi huo uliopo kusini mwa Tanzania. 


Waziri wa Nishati ,Januari Makamba ameshuhudia makubaliano hayo yaliyofanyika jijini Arusha na kusema kuwa serikali na kampuni zilizogundua gesi hiyo zilianza majadiliano tangu Novemba mwaka jana Kwa kutumia wataalamu wa ndani na amefarijika kuona majadiliano hayo yamekamilika .

"Kutokana na nia ya serikali kuhakikisha majadiliano hayo yanamalizika mapema ,imeona umuhimu wa kupata mshauri mwelekezi mwenye uzoefu mkubwa katika miradi ya aina hiyo"alisema Makamba .

Alisema utaratibu wa kimataifa katika masuala ya majadiliano ya miradi mikubwa kama huu wa kusindika na kuchakata gesi asilia LNG, ushauri wa kitaalamu kutoka kampuni zenye uzoefu ni muhimu .


Alisema mchakato wa manunuzi ya Mshauri Mwelekezi ulifanyika Kwa mujibu wa Sheria na kanunu za nchi na kampuni mbalimbali zipatazo 20 zilijitokeza na baada ya mchujo wa kina ilipatikana kampuni hiyo ya Bekar Botts (UK)LLP ambayo imetiliana Saini na TPDC Kwa niaba ya serikali.

Waziri Makamba alisema majadiliano hayo na Mshauri Mwelekezi yanafanyika Kwa muda wa miezi sita hadi juni mwaka huu  na mradio huo unatarajiwa kuanza  baada ya miaka miwili ijayo na baada ya miaka mitatu hadi mitano gesi ya kwanza  itapatikani.


Alisema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa ikiwemo kuiwezesha Tanzania kuingia kwenye ramani ya Dunia ya nchi zenye ushawishi Kubwa kupitia Nishati  ,pia gesi hiyo itatumika kwenye viwanda vikubwa vya ndani na kuuza gesi nje ya nchi.

Hivi karibuni Rais Samia Suluhu Hassan aliiagiza wizara ya nishati ya Tanzania kukamilisha majadiliano na wawekezaji ili mradi huo uanze kutekelezwa. 

Tanzania inakadiriwa kuwa na futi za ujazo trilioni 57.54 za gesi asili ambazo uzalishaji wake utasaidia taifa hilo la Afrika Mashariki kupata faida lukuki za kiuchumi ikiwemo kuchangia ongezeko la kasi ya ukuaji wa uchumi hadi kuzidi asilimia 7 mwanzoni mwa mradi.  

Kuanza kwa ujenzi wa mradi huo wa LNG huenda ikiwa moja ya kete muhimu ya kisiasa na mafanikio kwa Rais Samia ambaye amerithi miradi mikubwa ya kimkakati ya kimaendeleo .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI