MBUNGE wa Jimbo la Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi ametoa milioni 49.7 kwa ajili ya shughuli za miradi mbalimbali ambapo fedha hizo ni za mfuko wa maendeleo ya jimbo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi fedha hizo, Prof. Ndakidema aliishukuru serikali kuu kwa kutoa fedha hizo ambapo zitatumika katika miradi ya maendeleo ndani ya kata zote 16 za jimbo hilo.
Mbunge huyo alisema kuwa fedha hizo zitatumika katika miradi 17 ya maendeleo huku akibainisha kuwa tangu awe Mbunge wa jimbo hilo kwa miaka miwili sasa ameshapokea kiasi cha milioni 100 ambazo ni fedha za maendeleo ya mfuko wa jimbo.
Alisema kuwa, kata zote 16 zilipeleka maombi ambapo miradi 30 ya maendeleo yenye thamani ya milioni 141.3 iliombewa hivyo hawakuweza kufikia lengo hilo na kupelekea kuchambua baadhi ya miradi ya kipaombele ambayo miradi ya vyoo katika shule za msingi na zahanati.
Miradi hiyo ni kata ya Uru shimbwe ilipewa milioni 3 kwa ajili ya ukarabati wa vyoo shule ya msingi Shimbwe, kata ya Uru kaskazini milioni 3 ukarabati vyoo shule ya msingi Msareni, kata ya Mbokomu milioni 3 ukarabati wa vyoo shule ya sekondari ya Tema.
Miradi mingine ni kata ya Kindi milioni 3 ukarabati wa vyoo shule ya msingi Kindi kati, kata ya Kibosho kirima milioni 3 ukarabati wa vyoo shule ya msingi Kibachini, kata ya Kibosho mashariki milioni 3 ukarabati wa vyoo shule ya msingi Omi, kata ya Kibosho kati milioni 4 ukarabati wa vyoo shule ya msingi Otaruni.
"Pia tumepeleka fedha kata ya Uru mashariki milioni 3 ukarabati wa vyoo shule ya msingi Mwasi, kata ya Kibosho magharibi milioni 2 ukarabati wa vyoo shule ya msingi Kiwei, kata ya Old moshi magharibi milioni 3 ukarabati wa choo cha ofisi ya kata" alisema Mbunge Ndakidemi.
Aliongeza kuwa " kata ya Mabogini milioni 3 ukarabati wa vyoo katika jengo la kujifungulia mama zahanati ya Mabogini, kata ya Kibosho magharibi milioni 1 ukarabati wa ofisi ya kata, kata ya Okaoni milioni 3 ukarabati wa barabara ya Mloe yenye urefu wa kilomita 2".
Kata nyingine ni kata ya Kimochi milioni 3 ukarabati wa bwalo shule ya msingi Moo, kata ya Uru kusini milioni 3 ukarabati ofisi ya kijiji cha Rau, kata ya Arusha chini milioni 3 ukarabati wa darasa katika shule ya msingi Mikocheni, kata ya Old moshi mashariki milioni 3 ukarabati wa bweni la wasichana shule ya sekondari ya Meli.
Mwisho..
0 Comments