Wakulima wa matunda hususan wa zao la embe wametakiwa kutumia maabara ya kupima udongo ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) ili kuwa na uhakika wa aina ya udongo uliopo kwenye shamba husika na kuchukua hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kuongeza rutuba ambayo itamuwezesha mkulima kupata mazao mengi na bora.
Rai hiyo imetolewa leo na Naibu Mkuu wa Taasisi, Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Prof. Patrick Damson Nsimama alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja yaliyoratibiwa na DIT kupitia Mradi wa Utafiti wa maswala ya Kilimo ujulikanao kama ADEMNIA.Mafunzo hayo ni ya utunzaji wa zao la embe kwa wakulima wa zao hilo iliyofanyika katika shamba la maembe la KOGA lililopo Mkuranga Mkoani Pwani linalomilikiwa na mkulima Dkt. Salim Diwani."Nitafarijika sana kusikia ushuhuda wa kuongezeka kwa mavuno ya zao la embe kutokana na taarifa ya tathmini kutoka maabara ya kupima udongo ya DIT kuhusu eneo linalofaa kwa ulimaji wa zao hili lak8ni pia niwaase wakulima wengine kutumia maabara yetu kupima udongo kabla ya kuingia kwenye kikimo," amesema Prof. Nsimama.
Amesema kwamba katika ekari moja ana miti ya embe 70 na kwa kipindi chote hicho amekuwa akivuna maembe 14,200 kwa ekari moja.
Akizungumzia Mradi w ADEMNIA, Mratibu wa Mradi huo Dkt. Joseph Matiko alisema Mradi huo ni wa miaka 5 na unafadhiliwa na Serikali ya Norway lengo kuu la mradi huu ni kuboresha huduma za kilimo kwa kupambana na wadudu waharibifu wa mazao kwa kutafiti namna bora ya kupambana na wadudu waharibifu kama vile kutengeneza mitego ya kuwanasa wadudu hao kielektroniki.
Akitoa mada kuhusu udhibiti wa inzi wa embe na utunzaji wa zao hilo baada ya kuvunwa, msimamizi wa shamba hilo Bwana Hamadi Mkopi alisema wadudu wanaosumbua katika kilimo cha matunda ni wengi ila katika zao la embe mdudu hatarishi ni inzi ajulikanaye kwa jina la kitaalam Batrocella-Dosaris ambaye hapa nchini aligunduliwa mwaka 2003.
Aidha, ameeleza kuwa inzi huyu huharibu kati ya asilimia 50 hadi 80 ya zao la embe na juhudi za kumdhibiti inzi huyu kwa kutumia mitego ya asili zimeonyesha mafanikio ya kuridhisha
Mafunzo hayo yamehudhuriwa na wakulima 78 kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Arusha na Kilimanjaro.





0 Comments