Benki ya ushirika Mkoani Kilimanjaro (KCBL) imetoa bajaji 22 za mkopo kwa vijana wajasiriamali zenye thamani ya shilingi milioni 150 lengo likiwa ni kuwainua vijana hao kiuchumi......Na Rehema Abraham
Akikabidhi bajaji hizo msatahiki meya wa manispaa ya Moshi Mhe. Juma Raibu ameipongeza benki hiyo kwa jitihada walizozionesha ya kuendeleza uchumi na kusimamia changamoto zinazohusiana na wananchi wa Moshi.
Aidha amesema kuwa benki hiyo imekuwa benki ya kipekee kwa kujali maisha ya wananchi hususani wakulima.
"Benki hii kwa miaka ya nyuma ilikuwa imeyumba sana lakini niipongeze bodi ya wakurugenzi pamoja na meneja kwa kuamua kwamba benki hii inasonga mbele"Alisema Juma.
Amesema kuwa baadhi ya vijana wengi wamekuwa hawajitambui kwani wamekuwa wakiamini katika kupata bila kutafuta ,hivyo wamekuwa wakijiingiza katika unywaji wa pombe ,na uvutaji wa bangi pamoja na Mambo yasiyokuwa ya msingi.
"Nawapongeza vijana wote Hawa walioamua kujitokeza na kuamua kujiajiri kupitia benki hii ya KCBL ,na hii iwe Chachu kwa wengine , haiwezekani Baadhi ya vijana kuendelea kuamini Kuna kupata fedha bila kufanya kazi"Alisema
Hata hivyo amewataka vijana hao kusimamia bajaji Pamoja na kutumia Kama ilivyo kusudiwa na sio kubebea bidhaa za magendo Kama bangi na mirungi kwani kwa kufanya hivyo haitaleta faida Bali wataishia kukamatwa na kuwekwa ndani na kusababisha hasara.
Kwa upande wake meneja wa benki hiyo ya ushirika ya KCBL Godfrey Ng'urah
amesema kuwa utoaji wa bajaji hizo upo katika awamu ya pili ambapo thamani za bajaji hizo ni fedha kiasi Cha milioni mia moja na na hamsini zilizotolewa kwa vijana 22 ili kuhakikisha kuwa wanaleta huduma jumuishi za kifedha .
Amesema kuwa yapo makundi mahususi yaliyoachwa katika sekta ya fedha kwani wamekuwa hawapati huduma benki na Wala hawafikiriwi lakini na wao wanahitaji mikopo itaakayowasidia kusimama kwa miguu Yao wenyewe .
"Kama ambavyo tunangalia secta ya ushirika kuhakikisha kwamba wakulima wanapata masoko ya bidhaa na mavuno wanayovuna kwa Kila msimu katika secta ya kahawa ,tunafanya hivyohivyo katika jamii "Alisema Ng'urah.
Hata hivyo Amesema kuwa mchakato huo ni mkakati wa kuleta huduma jumuishi wa kuleta fedha kwa makundi maalum hasa Yale yaliyosahaulika Kama vijana waliomaliza masomo katika ngazi mbalimbali na kutoweza kuajiriwa wala kujiajiri katika nyanja mbalimbali .
0 Comments