Header Ads Widget

WANASWA NA NYAMA YA PUNDAMILIA ,NGOZI NA MKIA


Mwandishi wetu,MDTV Babati

 Mtuhumiwa wa ujangili Elias Misioyo mkazi wa kijiji cha  Kakoi , wilaya ya Babati mkoa Manyara amekamatwa akiwa na nyara za serikali na Nyama ya pundamilia,ngozi na mkia

Mtuhumiwa huyo amekamatwa katika operesheni za kupambana na majangili, katika eneo la ikolojia ya hifadhi ya Taifa ya Manyara- Tarangire na kikosi maalum ambacho kinaundwa na askari wa hifadhi ya jamii ya burunge ,Chemchem association na kikosi za kuzuia ujangili(KDU).

Mkuu wa kikosi cha kuzuiwa ujangili(KDU) Kanda ya Kaskazini Peter Mbanjoko, alithiitisha kukamatwa Kwa mtuhumiwa huyo Leo 1 Novembea 20 21.

Mbanjoko amesema kukamatwa Kwa mtuhumiwa huyo ambaye tayari amekabidhiwa Polisi ni kazi nzuri ambayo imefanywa na askari ,WMA na Chemchem ambao wamewekeza katika eneo hilo.

Askari wa Taasisi ya chemchem, Hamis Chamkulu amesema ilitoka na kupata taarifa zake muda mrefu akijihusisha na ujangili.

Taasisi ya chem chem ambayo imewekeza hoteli za kitalii na kufanya utalii wa picha katika eneo la burunge WMA imekuwa na mfuko maalum wa kupambana na ujangili ambapo kwa mwaka sh 400 milioni zinatumika  kufanya operesheni.

Mfuko huo unashirikiana  Askari ya Burunge WMA,askari ya kikosi maalum cha kupambana na ujangili kanda ya kaskazini(KDU) na  askari wa hifadhi ya Taifa ya tarangire  na kikosi cha askari wa ulinzi wa chemchem.

Wakati  huo huo, matukio ya uvamizi katika maeneo ya mapito ya wanyama katika eneo la ikolojia ya Tarangire - Manyara yameongezeka hali ambayo inaongeza  matukio ujangili.

Hata hivyo, licha vikao kadhaa baina ya Viongozi wa  wizara ya Maliasili ,halmashauri ya Babati lakini bado Suluhu ya uvamizi wa maeneo ya mapito ya wanyama haijapatikana.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI