Header Ads Widget

NGOME YA WANAWAKE ACT YAVUNJWA

Halmashauri Kuu ya Taifa ya ACT Wazalendo imeivunja Ngome ya Wanawake Taifa katika kile kinachoelezwa kuwa imeshindwa kutimiza majukumu yake. mwandishi wa matukio daima anaripoti kutokea Dar Es Salaam

Hilo ni moja ya maazimio ya Halmashauri Kuu yaliyotangazwa leo Novemba 1, 2021 na Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano kwa Umma, Janeth Rithe kwa waandishi wa habari. 

Rithe alisema  badala yake, Kamati Kuu imeunda Kikosi kazi cha Ngome ya Wanawake Taifa kitakachoongozwa na Pavu Abdallah (mwenyekiti), Wakili Bonifasia Mapunda (katibu) na wajumbe watakuwa ni Halima Ibrahimu, Annemerystella Mallaki na Sevelina Mwijage. 

Kamati Kuu kwa mujibu wa madaraka yake chini ya Ibara Katiba 79(1)(x) imevunja uongozi wa kitaifa wa Ngome ya Wanawake kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake "

Maazimio mengine ya Halmashauri Kuu ni pamoja na kutangazwa rasmi kwa nafasi ya Mwenyekiti wa chama Taifa iliyoachwa wazi na Marehemu, Seif Sharif Hamad aliyefariki dunia Februari 17,2021.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho cha pili kwa ukubwa kwa mujibu wa Katiba ya ACT Wazalendo ilitangaza rasmi uchaguzi wa nafasi za Mwenyekiti wa Chama Taifa, Makamu Mwenyekiti Zanzibar, na nafasi moja ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu kufuatia kujiuzulu kwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar Ndugu Juma Duni Haji. 

"Kwenye barua yake ya kujiuzulu aliyomwandikia Katibu Mkuu wa Chama tarehe 30 Oktoba 2021, Ndugu Juma Duni Haji aliweka bayana kuwa amejiuzulu nafasi hiyo kwa sababu ana nia ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Taifa, hivyo amejiuzulu ili nafasi hizo mbili zitangazwe pamoja. Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chama, Makamu Mwenyekiti wa Zanzibar na uchaguzi wa nafasi moja ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ambayo nayo ipo wazi utafanyika kupitia Mkutano Mkuu wa Chama Taifa utakaofanyika tarehe 29 Januari 2021." alisema  


 Rithe aliwaeleza waandishi kuwa Halmashauri Kuu ya Chama Taifa imeazimia kwa kauli moja kuwa Chama kiendelee kwa kasi zaidi kuipigania Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi.

Halmashauri Kuu imeazimia kuwa Chama kitakuwa mstari wa mbele kupigania mageuzi ya kiuchaguzi (electoral reforms) ili chaguzi zijazo kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (chini ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi-NEC) na zile za Zanzibar (chini ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar-ZEC) ziwe huru, za haki na za kuaminika (free, fair and credible elections).

Pia imepongeza mwenendo wa Chama kuendelea kuisimamia Serikali na kupigania maslahi ya makundi mbalimbali kwenye jamii. 

Halmashauri Kuu pia iligusia suala la Wamachinga, ambapo imeagiza viongozi wa Chama wa Kitaifa na Mikoa kupaza sauti kuwatetea Wamachinga kwa kutoa majawabu na mapendekezo ya changamoto zao.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI