Header Ads Widget

MWALIMU MKUU WA KARATE KUWASILI NCHINI MWEZI UJAO

 


Mwalimu  Mkuu wa Sanaa ya Kujilinda ya Jundokan Karate nchini Tanzania Sensei Rumadha Fundi (pichani mbele) anatarajiwa kuwasili nchini mwezi ujao ambapo Pamoja na mambo mengine atawatahini wanafunzi kadhaa wa mtindo huo na kuwapandisha daraja. 


 Msemaji wa Jundokan Karate Tanzania, Sensei Wahid Wacha, amesema kwamba Sensei Fundi alikusudia kuja Tanzania toka mwaka  jana (2020), lakini kutoka na vikwazo mbalimbali viliyojitokeza na kusababishwa na janga la Corona duniani alishindwa kuja nchini. 


 Sensei Wahid amesema Sensei Fundi, ambaye ni Mtanzania na muwakilishi wa Sensei Kancho Yoshihiro Miyazato wa kiongozi wa Jundokan Honbu Dojo duniani yenye makao yake Okinawa, Japan, na ndiye mwenye mamlaka kwa Dojo za Tanzania za mtindo huo pamoja na kusimamia mitihani ya Daraja za juu kwa Dojo zote za Jundokan Tanzania. 


 Akielezea ratiba ya ziara hiyo, Sensei Wahid ameeleza kwamba Mwalimu huyo Mkuu wa Jundokan Tanzania anatarajiwa kuwasili nchini Ijumaa Desemba 3, 2021 usiku na kwamba siku ya pili yake Jumamosi ya Desemba 4, 2021 Sensei atafanya mazoezi na wanafunzi wake katika Jundokan So Honbu Dojo katika Shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Dar es salaam. 


 “Siku ya Jumapili Desemba 5, 2021 tutakuwa na mazoezi ya pamoja alfajiri na baadae jioni na siku ya Jumatatu Desemba 6, 2021 pia kutakuwa na Mazoezi ya asubuhi na Jioni. 


 “Siku ya Jumanne na Jumatano (Desemba 7 na 8) Sensei Fundi atakuwa nje ya Dar esalaam kwa shughuli za binafsi za kifamilia na kurejea Dar es salaam siku ya Alhamisi Desemba 9 ambapo yake ataendelea kufanya mazopezi na wanafunzi wake. Ijumaa Desemba 10 itakuwa siku ya mapumziko”, amefafanua Sensei Wahid. 


 Amesema siku ya Jumamosi Desemba 11 kutakuwa na mitihani kwa wanafunzi waandamizi hususan wataopanda madaraja ya Shodan (mkanda mweusin daraja la kwanza) Nidan (mkanda mweusi daraja la pili) na Sandan (mkanda mweusi daraja la tatu). 


 “Muda wa kufanya mitihani utaamuliwa kulingana na muitikio na kuwasili kwa wenzetu wa mikoani. Inaweza mitihani ikafanyika asubuhi, au ikafanyika asubuhi na jioni. Hii ni kwa ajili ya kumpa nafasi kila mmoja kupata haki yake ya kutahiniwa”, amefafanua.


 Amewataka wanafunzi wote wanaotakiwa kufanya mtihani wajitahidi kutokosa katika kipindi hiki haswa ukizingatia kuwa kwa ratiba zake, Sensei Fundi huwa ataweza kuja tena kuanzia mwaka mmoja na nusu mpaka miwili baadaye kwani nafasi yake ya kusafiri hutegemea ruhusa kazini, kuhudhuria Semina za Jundokan nchi mbalimbali za nje Pamoja na mambo mengine. 


 Amewataka wale wote wanaotakiwa kufanya mitihani na ambao bado hawajawasilisha majina yao wawasiliane nae Sensei Wahid Makao Makuu ya Jundokan au masensei wengine ili kupata taarifa na maelekezo muhimu. 


 Sensei Wahid amesema siku ya Jumapili Desemba 12, 2021 mapema asubuhi kutakuwa na mazoezi ya mwisho na Sensei Fundi na baadae kutakuwa na mazungumzo na vyombo vya habari, kabla ya chakula cha pamoja, na kwamba Sensei Fundi ataondoka kuelekea Marekani anakoishi na kufanya kazi siku ya Jumatatu Desemba 13. 


 “Sensei Fundi amekuwa akitenga muda wake mwingi kwa hali na mali ili kuwa na sisi kimafunzo na mwishowe kuwa na sisi kimazoezi hapa nchini. 


Ame kuwa akifanya hivyo kwa kujitolea na gharama zake binafsi, mbali ya Zile ziara anazozifanya nchi mbali mbali katika makongamano ya Jundokan ikiwepo na Japan. Hivyo ndugu zangu tusiache fursa hii ya kuwa naye pamoja kimazoezi”, amemalizia Sensei Wahid. 


 Kiongozi huyu mkuu wa Dojo la Shibu cho Jundokan Karate Tanzania ni mwenye daraja la GODAN (mkanda mweusi daraja la tano) alilopokea mwaka 2019 toka kwa Sensei Kancho Miyazato, Mkuu wa karate mtindo wa Jundokan Goju Ryu Duniani. 


Sensei Fundi amekuwa Mtanzania wa Kwanza kufika ngazi hiyo ya juu yenye uthibitisho toka makao makuu ya Jundokan Goju Ryu Karate do huko Okinawa, Japan.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI