Header Ads Widget

Rais Samia Katika Mkutano wa COP26 nchini Glasgow, Scotland

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akielekea kwenye ukumbi wa Mkutano kwa ajili ya kuhudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa utakaojadili athari za mabadiliko ya tabianchi (COP26) unaofanyika Glasgow, Scotland leo tarehe 01 Novemba, 2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi Green Climate Fund (GCF) Yannick Glermarec kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa 26 wa Umoja wa Mataifa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiagana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Kupambana na Mabadiliko ya Tabianchi Green Climate Fund (GCF) Yannick Glermarec mara baada ya kuzungumza nae


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera kabla ya kuanza kwa Mkutano


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Malawi Dkt. Lazarus Chakwera


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha na Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Boris Johnson (kushoto) pamoja na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (kulia)

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI