Header Ads Widget

WATU WANNE WAFARIKI DUNIA KWA AJALI


Watu wanne wamefariki dunia Mkoani Iringa katika matukio mawili tofauti likiwemo la dereva Simoni Runocho (33) mkazi wa Kinyanambo A kumgonga mtoto wa darasa la tatu maeneo ya barabara kuu Iringa - Makambako wilaya ya Mufindi.
mwandishi wa matukio daima anaripoti.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Juma Bwire alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea mnamo tarehe 21 Oktoba majira ya saa 11 na nusu jioni.

Kamanda Bwire alisema mtuhumiwa alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Noah yenye namba za usajili T 432 CGN alimgonga mtembea kwa miguu aitwaye Careed Dorati (8) mwanafunzi wa shule ya msingi Amani iliyopo Mafinga na kumsababishia kifo akiwa njiani kupelekwa hospitali.

Kamanda alisrma kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kushindwa kuchukua tahadhari kwenye kivuko cha watembea kwa miguu ambapo dereva wa gari amekimbia na juhudi za kumtafuta zinaendelea. 

katika tukio lingine lililotokea Octoba 20 gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 319 DVN mali ya Assif Asraf lililokuwa likiendeshwa na Hassan Mohamed (37)  huko maeneo ya Sao Hill barabara kuu ya Iringa- Makambako,  akitokea Sumbawanga kuelekea Dar Es Salaam aligongana na gari aina ya Mark X yenye namba za usajili IT 8638 mali ya NM FREIGHT TANZANIA LTD iliyoko mkoa wa Dar Es Salaam lililokuwa likiendeshwa na Mbaraka Juma (38) na kusababisha vifo vya watu watatu na majeruhi mmoja.

Hata vivyo Kamanda Bwire alisema kuwa miili ya marehemu imetambulika kwa majina ambapo ni Justine Godfrey (37) mkazi wa Njombe, Abdallah Shaban (45) mkazi wa Buza pamoja na dereva wa IT huku majeruhi ni Sesilia Edwin (22) mkazi wa Kyela mkoani Mbeya. Miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Mji wa Mafinga.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI