Wananchi wa kitongoji cha Mikoroshini kata ya Minepa eneo la Iluma Wilayani Ulanga Mkoani Morogoro wameiomba serikali kukidhibiti kikundi cha watu wanaojiita mgambo maarufu kama VILAPU ambao wanafanya uvamizi katika makazi ya wananchi hao na kufanya uharibifu ikiwa ni pamoja na kuwapiga,kupora kisha kuchoma nyumba zao.
Wakizungumza na wandishi wa habari wananchi hao walisema Vilapu wamekuwa wakiwavamia usiku kisha kuanza kuwapiga huku wakijifanya ni askari wa Wanyamapori.
Wananchi hao walisema kufuatia kazia hiyo wametoa taarifa kwa baadhi ya viongozi akiwemo diwani lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa ya kudhibiti kikundi hicho kinachojulikana kwa jina la VILAPU.
Kufuatia sakata hilo tulimtafuta mbunge wa Jimbo la Ulanga Salim Hasham ambapo alithibitisha kuwepo kwa matukio ya wananchi wanaoishi maeneo Iluma kuhalibiwa mali zao ikiwa ni pamoja na kupigwa na VILAPU.
Kwaupande wake Katibu tawala Wilaya ya Ulanga Abraham Mwaikwila aliwataka watu wanaofanya vitendo vya uvunjifu wa amani kwa wananchi hao kuacha mara moja huku akiahidi kulifanyia upelelezi wa kina jambo hilo.
0 Comments