Mkuu wa wilaya ya Longido Nurdin Babu amesema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi yanachochea kuongezeka kwa changamoto kati ya binadamu na wanyama ambapo wameshuhudia yakileta madhara kwa wananchi waishio pembezoni mwa hifadhi mbalimbali. mwandishi wa matukio daima Namnyaki Kivuyo anaripoti kutokea Arusha
Babu aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha wadau wa mradi wa mabadiliko ya tabia ya nchi kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela, mkutano uliofanyika mkoani Arusha ambapo alisema kuwa mabadiliko ya tabia ya nchi imekua ni changamoto kubwa kwa maisha ya binadamu na maendeleo ya kiuchumi ya mtu mmoja mmoja na na nchi kwa ujumla.
Alisema kuwa watu wamekuwa wakiuawa na wanyama pori na ni wiki chache tu walipokea taarifa za kuuawa kwa mwanakijiji wilayani Same lakini pia wameshuhudia mifugo ikiuawa pamoja na mazao kuharibiwa vibaya na wanyama pori na yote hayo yanasababishwa na mabadiliko ya tabia ya nchi.
“Wanyama wanakosa maji na chakula porini jambo linalosababisha wanasogea karibu na makazi ya watu lakini nao binadamu kwa kutafuta ardhi yenye rutuba kwa ajili ya kilimo na mifugo wanajikuta wanasogea zaidi karibu na maeneo ya hifadhi jambo linaloleta muingiliano na migogoro Kati ya binadamu na wanyama pori,” Alisema Babu kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Arusha
Alisema kuwa mradi wa mabadiliko ya tabia ya nchi umewezesha ujenzi wa malambo ambao utasaidia kupunguza muingiliano kati ya binadamu na wanyama hasa pale yanapopatikana maji ya kutosha kwaajili ya wanyama pori na mifugo ambapo zimetengenezwa pampu za maji zinazotumia umeme wa jua, wameweka uzio kuzuia wanyamapori kuvamia maeneo ya makazi na mashamba.
“Mradi huu umetekelezwa kwa muda mfupi na ipo katika kiwango kinachokidhi vigezo na mahitaji na kwakweli binafsi na kwa niaba ya serikali niwashukuru kwa kujitolea katika kukamislisha kazi hii nafahamu wapo waliofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mradi unakamika,” Alieleza.
Aidha aliwaagiza wananchi waliopo katika maeneo ambayo miradi hiyo imetekelezwa kuhakikisha wanatunza miradi hiyo na kutumika kukidhi malengo yaliyokusudiwa kwani WWF wamewasaidia lakini hawategemei warudi kuja kusimamia miradi hiyo kwani kwa sasa ni ya kwao hivyo wailinde,waihudumie na kuitunza ili iwasaidie kupunguza makali ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Aliambiwa kuwa mradi huo unafikia mwisho lakini bado wanahitaji msaada mwingine katika kuhakikisha wanaibua miradi mingine ili wananchi waweze kunufaika lakini kwa wakati mwingine hizi WMA zisimame zenyewe kusiwe na visingizio kwani jamii nyingi zinategemea maliasili kiuchumi na kimaendeleo.
kwa upande wake meneja wa mradi huo Novat Kessy alisema kuwa mradi huo unatekelezwa na shirika la uhifadhi wa mazingira (WWF) ambapo wamefanya mradi huo ili kuzijengea jamii uwezo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi ambapo katika maeneo ya Kaskazini madhara makubwa Ni ukame na wamekuja na mkakati wa kuwawezesha kukabiliana nayo.
Alisema jamii wanazofanya nazo kazi Ni wafugaji na wamekuwa wakitembea umbali mrefu kufuata maji ambapo wamewasaidia kwa kuwajengea mabwawa makubwa(Malambo) kwani wamekuwa wakipata mvua chache na ili maji yake yasipotee mabwawa hayo yanatumika kwa kuhifadhia maji yatayotumika wakati wa ukame.
Sambamba na hayo pia tunazijengea jumuiya za wanyapori uhifadhi za kijamii uwezo wa kupanda miti pamoja na kuwapa mafunzo ya malisho yanayokabiliana na ukame ambapo wamepewa mbegu za malisho na mradi huu unafadhiliwa Ujerumani ambapo ni mradi uliotekelezwa kwenye maeneo yanayozunguka hifadhi
Profesa Noah Sitati mtaalamu wa masuala ya wanyama pori alisema kuwa hadi sasa Kuna maji katika maeneo yote ambayo wamefanyia mradi huo uliogharimu uro milioni 5.2 kwa Tanzania na Kenya ambapo Tanzania wamenufaika kwa asilimia 51 na Kenya kwa asilimia 49.
Alifafanua kuwa kwa kumalizika kwa mradi huo umepelekea kuanzishwa kwa mradi mwingine wa miaka mitatu utakaonza January 2022 ambao utahusika na masuala ya Tembo na maradi huo unaanzishwa mahususi kutokana ongezeko kubwa la idadi ya tembo na utagharimu uro milioni 10.2 ambapo pia utatekelezwa Kenya matumizi ya kwa asilimia 49 na Tanzania kwa matumizi ya 51.
0 Comments