Header Ads Widget

MAADHIMISHO YA WIKI YA POSTA DUNIANI YATAKIWA KUTUMIKA KUREJESHA MATUMAINI KWA WANANCHI KUHUSU HUDUMA ZA POSTA

 


Na Hamida Ramadhani, Dodoma 


KATIKA Kuadhimisha kilele cha Maadhimisho ya wiki ya Posta Duniani Serikali imetoa wito kwa uongozi wa Shirika hilo kutumia maadhimisho hayo kurejesha matumaini kwa wananchi kuhusu huduma za posta.


Wito huo umetolewa leo jijini Dodoma na Makamu Mkuu wa Rais  Philip Mpango ambaye alikuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo ambapo amewataka kuongeza jitihada katika kutangaza huduma zake kote duniani na kutumia zaidi lugha ya kiswahili.


"Rudisheni matumaini kwa wananchi  kuhusu huduma zenu za posta  mnazozitoa kwani ni ukweli usiopingika wananchi walishashoshwa na kukata tamaa juu ya shirika lenu ,"amesema Dkt Mpango


Aidha kwa upande wake Waziri  wa Habari Mawasiliano na Keknolojia ya Habari Dkt Ashatu Kijaji ameshukuru na kupongeza jitihada zinazofanyika na shirika hilo pamoja na kusema kuwa anaamini wananchi kote nchini wamefahamu zaidi kuhusu huduma zinazotolewa na shirika hilo kupitia maadhimisho hayo.


Amesema umoja wa duniani ni chombo cha umoja wa mataifa UN chenye jukumu la kuendeleza huduma  za posta hapa duniani.


"Tumefanya maadhimisho siku nne mfululizo huku tukishirikiana na wadau mbalimbali katika sekta ya posta na nje ya posta  nia ni kuonyesha  Umma  umuhimu wa huduma za posta," amesema Dkt Kijaji


Naye Posta Masta Mkuu  Shirika Macriss Mbodo,amesema lengo la Maadhimisho hayo ni kutambua na kuboresha zaidi huduma za posta kote duniani na kuongeza kuwa shirika hilo limejipanga vyema katika kuboresha huduma ikiwa ni pamoja na kuongeza miundombinu rafiki ya kazi.


Kilele cha maadhimisho hayo kitaifa yamefanyika jijini Dodoma huku mgeni rasm akiwakabidhi  vyeti  washiriki wa uandishi wa barua pamoja na vitendea kazi kwa kama,magari na pikipiki kwa uongozi wa shirika.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI