Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassani ameipongeza Twiga Stars kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya COSAFA Wanawake 2021.
Kupitia katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Samia amesema kuwa ubingwa huo ni heshima kubwa kwa taifa na chachu kwa vijana kushiriki michezo.
"Naipongeza timu yetu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya COSAFA Wanawake 2021. Ubingwa huu unatuletea heshima, unaitangaza nchi yetu na kutia chachu kwa vijana wetu kushiriki michezo. Naipongeza TFF na wote walioshiriki kuiandaa timu yatu"
Twiga Stars imetwaa ubingwa huo kwa kuifunga timu ya Malawi bao 1-0 katika Mashindano ya COSAFA ya Wanawake yaliyofanyika nchini Afrika Kusini.
Goli la Twiga Stars katika mchezo huo limefungwa na Enekia dakika ya 64.
0 Comments