Na Fatma Ally,MDTV Dar es Salaam
Jumuiya ya watoa huduma katika Sekta ya mafuta na gesi (ATOGS) leo imekutana na wadau wapya katika Sekta hiyo kwa lengo la kujuana na kuwakaribisha wanachama wapya ambao wamejiunga hivi karibuni katika jumuiya hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti na Mwanzilishi wa jumuiya hiyo, Abdulsamad Abdulrahim amesema kuwa, watu wamekua na imani na jumuiya hiyo kutokana na mambo wanayoyafanya.
"Watu wamechokua kukaa katika vyama ambavyo havina tija wala muelekeo, jumuiya hii imetekeleza mambo mengi kuhakikisha wafanyabiashara wanafanya kazi katika mazingira rafiki"amesema Abdulsamad.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Magare Campan Limitted, Mabula Magangila amesema lengo la kujiunga na jumuiya ya Atogs ni kupata fursa mbalimbali za miradi ya kimkati katika Sekta ya gesi na mafuta.
Amesema kuwa,wana matawi katika nchi mbalimbali ikiwemo South Afrika, DRC Congo pamoja na Tanzania, ambapo wamekua wakifanya kazi kwa uweledi zaidi katika huduma wanazozitoa.
Ameongeza kuwa, jumuiya ya Atogas imekua ikifanya kazi ya kutangaza biashara za watanzania pamoja na kukuza biashara kwa ajili ya watanzania kama kauli mbiu yao inavosema.





0 Comments